Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko kutoka katika Mfuko wa GEPF akifafanua jambo kuhusu mafao yatolewayo na Mfuko wa GEPF katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arusha.
Mwanachama
mpya akipata maelekezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa GEPF kutoka kwa
Afisa wa GEPF Bi Jane Rutashobya katika maonesho ya wakulima ya
nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arusha
Afisa
Masoko Clement Oningo akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko wa Mafao
ya Kustaafu wa GEPF kwa wakazi wa jiji la Arusha waliofika katika banda
la GEPF.
Muonekano wa banda la GEPF katika viwanja vya nane nane jijini Arusha.Meneja
Masoko Aloyce Ntukamazina , Alitoa wito kwa wakazi wa Arusha
kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya nane nane ili kupata elimu na
faida za kujiunga na mfuko huo. “Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi
katika maonyesho haya na kuja kutembelea katika banda letu na kuweza
kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huu”alisema Ntukamazina.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...