Mwakilishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (kushoto) akisalimiana na baadhi ya Wanamichezo waliokuwa kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Juliana Yassoda akiwaelekeza jambo baadhi ya Wanamichezo waliwakirisha Tanzania kwenye Mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara walipowasilia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) Bw. Filbert Bayi akifurahia jambo na baadhi ya wanamichezo walikuwa wamewakilisha nchini katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Glasgow Scotland mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
heshima sawa..ila medals ziko wapi tuache porojo watanzania wenzangu
ReplyDeletemdau
Wameonyesha heshima? Kwani walienda kuonyesha heshima au kucheza na kuleta medals? Heshima gani wakati bondia wetu mmoja alijificha chooni hakutaka kupigana akiogopa kushindwa? Wenye heshima walishinda na kuleta medali katika nchi zao sio hao wa kwetu....JAMANI HATA MEDALI MOJA? AIBU....ingekuwa nchi nyingine wangejiuzulu wakubwa wote wa idara ya michezo...lakini kwetu porojo nyingi.
ReplyDelete