Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST ) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano ya Wajiolojia Afrika na wanasayansi vijana Duniani, Profesa Abdulkarim Mruma (katikati) akisisitiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na mkutano wa tatu wa vijana wanasayansi kutoka nchi mbalimbali duniani. Makongamano hayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 11- 16 Agosti, 2014 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud. Wengine, kwanza kulia ni Mwenyekiti wa mtandao wa Vijana wanasayansi kwa upande wa Tanzania Steven Nyagonda, Rais wa Vijana wanasayansi Duniani Meng Wang na Katibu wa Kamati ya Maandalizi, Profesa Nelson Boniface.
Rais wa Wanasayansi Vijana duniani, Meng Wang (wa pili kulia) akiongea jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuelezea kuhusu mkutano wa tatu wa wanasayansi vijana kutoka nchi mbalimbali duniani, kulia ni Mwenyekiti kongamano la vijana wanasayansi upande wa Tanzania Steven Nyagonda, wengine wanaosikiliza ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Katibu wa kamati ya maandalizi, Profesa Nelson Boniface.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wakitoa taarifa kuhusu kufanyika kwa kongamano la 25 la Wajiolojia Afrika na kongamano la tatu la wanasayansi vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani. Kushoto ni Michael Msambi mjumbe wa kamati ya maandalizi na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya makongamano hayo, Profesa Abdulkarim Mruma (kulia).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...