Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi,Abdallah Bulembo (katikati) akiwasili katika viwanja vya karimjee jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuungana na wasanii kwenye dua maalum ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki.Kulia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere.
Msanii wa vichekesho ambaye pia ni muinjilisti kwa sasa Emanuel Mgaya Maarufu kama Masanja Mkandamizaji akiongoza dua kwa upande wa wakristo huku Msanii Jacob Stephen JB akiwa ameishikilia Biblia.Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum ambaye aliongoza dua kwa upande wa waislam,katika shuguli hiyo ya kuwaombea Wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika jana kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam.
 Baadhi ya wadau wa Filamu nchini wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuwaombea Dua Wasanii wote waliotangulia mbele ya haki (waliofariki) iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee,jijini Dar es salaam jana.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Alhaj Mussa Salum akijadiliana jambo na baadhi ya wadau walioshiriki kwenye dua hiyo.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity,Steven Mengele maarufu kama Steve Nyerere akipeana mkono na watu mbali mbali baada ya kumalizika kwa dua ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele ya haki,iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Nawapongeza nyote kwa jumla kwa kulifikiria hilo na kulitendea kazi, nanyi In Sha Allah, MOLA atawalipa fungu lenu. Mmefanya jambo jema, la manufaa na lenye kheri ndani yake kwa kuwakumbuka wenzenu wote waliotangulia mbele ya haki. In Sha Allah, Mwenyeez Mungu awarehem na awaghufirie kwa yote huko waliko na kuwapumzisha palipo pema peponi - AMEEN.

    Steve vazi limekukubali, umependeza Masha Allah!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...