Watu  zaidi ya 17 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa  baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji  cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Ajali hiyo imetokea leo hii jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi ( Day-worker).Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.

Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP). Suzana Kaganda ili kuzungumzia ajali hiyo bado zinaendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tatizo la hawa madereva wa tz hawana mafunzo ya udereva mtu kwa sababu anajua kuingiza gea moja mpaka tano ndio imetoka, reseni zao za kuchakachua tu ukitoa rushwa tu reseni unapata; serikari fanyeni msako kwa madereva wanaomiliki reseni muwaulize kama wamefanya mafunzo ya udereva na chuo gani wamepitia, wengi wao walikua ni wapiga debe

    ReplyDelete
  2. Madereva sijui tusemeje sasa hizi ajali zimezidi watu wanapoteza maisha tukumbuke kuwa makini tukiwa barabarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...