Vijana wawili wamechomwa moto katika eneo la Tabata Liwiti wakituhumiwa kuiba pochi ya mwanamke katika eneo hilo,Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa lilitokea asubuhi ya jana (Jumamosi) ambapo walikuwa watatu wakafukuzwa na watu mbalimbali.

Alisema kuwa walipokamatwa walipigwa na kisha kuchomwa moto.

"Matukio haya yamekuwa yakitokea mara kwa mara hapa Tabata na wezi wanaoiba kwa kutumia pikipiki wamekuwa ni kero kubwa sasa na kila wakikamatwa na kupelekwa vituoni wanaachiwa na Polisi ila kwa sasa wananchi wameamua kutumia sheria mkononi."
Askari kanzu wa Jeshi la Polisi wakipakia kwenye gari mabaki ya miili ya vijana wawili waliotuhumiwa kuwa ni wahalifu wa uwizi waliochomomwa moto jana maeneo ya Tabata Liwiti,jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Wananchi wakazi wa Tabata Liwiti pamoja na Askari Kanzu wa Jeshi la Polisi wakiangalia mabaki ya miili ya vijana wawili waliosadikiwa kuwa ni wahalifu wa uwizi waliochomomwa moto jioni maeneo ya Tabata Liwiti,jijini Dar es salaam.
Hii ndio pikipiki waliokuwa wakiitumia wahalifu hao.
Picha na Evance Ng'ingo wa habari5blog

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Tanzania nchi ya amani na upendo!!

    ReplyDelete
  2. Polis kwa nini msifanye uchunguzi kwa waliohusika kuwachoma moto hao wezi na kuwachukulia hatua maana haya ni mauaji ya wazi tu na tukiacha yaendelee basi wezi wataendelea kuuawa bila ya kuchukuliwa hatua...Remember they are innocent until proven guilt.

    ReplyDelete
  3. Sheria za Haki za binadamu zazidi kuvunjwa kila siku! Watu wazidi kujichukulia sheria mkononi, Kairuki na Mwenzako mnaona hii??!! Wahusika wa haki za Binadamu Tanzania mnaona hii??!! Mnafanya nini kutoa elimu kwa wananchi juu ya maswala ya kujichukulia sheria mkononi??

    Kumbukeni ni Innocent until proven guilty.

    ReplyDelete
  4. This is a barbaric act.. should not be condoned by anyone. Your purse cannot be equated to someone's life. They should be arrested and taken to court and NOT killed in this manner. Shame on everyone that was involved..

    ReplyDelete
  5. ni pochi tu au kuna mengine ndani yake, just imagine angekuwa mwanao ,kaka,mjomba yako au ndugu yako unejisikiaje ,kila mtu afanye kazi yake kwa umakini zaidi

    police tujiimarishe zaidi kudhibiti uhalifu mtu anaweza kuitiwa mwizi kwa visa tu jamani

    wananhi jamani tutafakari kabla ya kuchukua hatua mbaya vyombo vya sheria vipo

    ReplyDelete
  6. Kosa la wizi sio kuuawa na kuchomwa. Watu wasijichukulie sheria mkononi.

    ReplyDelete
  7. Jaman uwiii hao vjana ni wa huku bgrn.. So so saaad..huo msiba wao wakat wa kuzika ilikuwa ni ishuuu watu wameibiwa ni balaa yan ni wahun kibao ilikuwa ni shida hatareer.. R.I.P. Chief

    ReplyDelete
  8. Tunaomba Serikali ianzishe kampeni ya kutoa elimu kwa jamii na pesa zitoke ktk wizara ya katiba na sheria pamoja na wizara ya mambo ya ndani ili haya mambo yasiendelee na yaishe. Wadau wengine ktk sekta hii wahusishwe pia.

    Sijisikii Amani kabisa nikiona haki za binadamu zinazidi kuvunjwa na wananchi wenyewe utadhani hii nchi haiendeshwi na sheria, Katiba au hakuna vyombo vya dola??!!

    Kuua binadamu mwenzako ni kosa kikatiba na kosa kwenye haki za binadamu. Wanatoa hukuma bila ata ya ushahidi!! na nani kawapa mamlaka ya kutoa hukumu ya kifo??!!

    Ndugu yangu Michuzi tunaomba hii mada uirudie na kuiweka tena mwanzo juu ya website ili wananchi tuitolee mada kiundani maana leo hawa kesho atakuja kuwa ndugu yetu.

    ReplyDelete
  9. Nikiangalia vizuri eti askari anacheka na wengine wanatazama tu, kwanini wasiwakamate walio wachoma na kuwaua wenzao? Si wamevunja sheria pia?

    Tukiacha polisi wamebaki wanacheka na kutazama hii hali itazidi kuendelea na wananchi watazidi kuvunja sheria na kujichukulia sheria mkononi...

    Kama raia wanaua raia wenzao basi Tanzania sio nchi ya Amani na Upendo wala Tanzania sio nchi ambayo inafuata sheria.

    Waziri wa Katiba na Sheria, Dr.Asha-Rose Migiro na msaidizi wako pamoja Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe fuatilieni maswala haya ili tubaki na Amani.

    Kumbukeni sisi ni binadamu na tupo kwenye civilised era na SIO wanyama ambao tunauana wenyewe kwa wenyewe pale tunapokoseana. Usipoziba ufa basi kumbukeni tutajenga ukuta kwa uzembe wetu wenyewe maana wananchi watazoea kuua na itakuwa kawaida kwao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...