Wazazi wana wajibu na ulazima wa kuhakikisha kwamba watoto wao wanawasimamia vyema katika kupata elimu bora itakayotoa mwanga wa kimaisha katika hatma yao ya baadaye. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akizunghumza na Uongozi wa Kamati ya Skuli, walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini Wilaya ya Kaskazini “A “ mara baada ya kuikagua na kuangalia maendeleo na changamoto zinazoikabili skuli hiyo. 

Balozi Seif alisema elimu ndio ufunguo pekee pekee utakaowapa njia watoto hao kukabiliana na mazingira ya kimaisha yanayokwenda kwa kasi na haraka ndani ya mfumo wa sasa wa sayansi na Teknolojia. 

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Kamati ya Uongozi ya Skuli hiyo kwa jitihada zake kubwa inazochukuwa kwa kushirikiana na walimu na kuleta maendeleo makubwa. Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya Wazee wa Skuli ya Sekondari ya Kinyasini Nd. Simba Haji alimuomba Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kufuatilia ahadi iliyotolewa na aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Mwisho wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kutafuta mbinu za kulitengeneza Jengo la madarasa manne la Skuli ya Msingi ya Kinyasini ambalo liko katika hali mbaya. 

Skuli ya Kinyasini ikiwa ni miongoni mwa skuli kongwe ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja iliasisiwa mnamo mwaka 1946 kwa Darasa la Quran na kuanza kwa darasa la kwanza mwaka 1947 lililoendelea hadi darasa la kumi na moja kwamba 1973.
Mwalimu Mkuu wa SDkuli ya Sekondari ya Kinyasini Mkoa wa Kaskazini Unguja Mwalimu Haroun Juma akimkaguza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefanya ziara fupi kuangalia maendeleo ya changamoto zinazoikabili Skuli hiyo.
Balozi Seif akibadilishana mawazo na walimu wa Skuli ya Kinyasini Sekondari alipokfanya ziara fupi skulini hapo.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Kinyasini Sekondari Haroun Juma akimuonyesha Balozi Seif Vikalio vilivyotengenezwa kwa zege ndani ya madarasa ya Sekondari ya skuli hiyo.
Balozi Seif akishangaa mabadiliko makubwa ya majengo ndani ya Skuli ya Sekondari ya Kinyasini ambapo ndipo alipoanzia kupata elimu ya msingi katika miaka ya 46. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Skuli ya Kinyasini Sekondari Nd. Simba Haji.
Balozi Seif akiangalia kisima cha Skuli hiyo ambacho kilipata hitilafu ya mafuta baada ya bomba la mafuta lka kituo cha Petroli kiliopo katibu na skuli hiyo kupasuka na kutembea katika miamba hadi eneo hilo la kisima. Kushoto ya Balozi Seif ni Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo ya Kinyasini Sekondari Mwalimu Haroun Juma.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizunguma na wazazi, kamati ya skuli, walimu na wanafunzi wa skuli ya sekondario ya Kinyasini mara baada ya kukaguzwa kuona maendeleo na chngamoto zinazoikabili. Picha na Hassan Issa wa –OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hivyo vikalio vya zege kwa darasani kidogo vinanipa mushkel, maana kuwa na madawati au viti na meza vilivyotengenezwa kwa mbao, vikawa darasani kuna maana na umuhimu wake, sio kuwa mradi tu wanafunzi wasikae chini, la khasha! Lakini tena kuwatengenezea hivyo vya zege visivyosogezeka wala kuhamishika ni sawa na 'miamba' (rocks) then pakajengwa darasa zikawa ndani kama vikalio. Japokuwa ni ubunifu na hatuwa nzuri ya kujikimu na tatizo hilo la uhaba wa madawati, sio kuwa navipinga, lakini 'considerations' ya hao watumiaji pamoja na 'risk assessments' za hilo zege, mana hapo umejigonga au kuangukia hapo kwa bahati mbaya, zege hilo, sidhani kama patakuwa na manusura, pia kukalia dawati na kukalia hiyo zege kuna tofauti kubwa sio almuradi tu mwanafunzi akae, hapana kila kitu ni lazima kiendane na mazingira, ubora na mahitaji yake husika na sio tu kurakhisisha kazi.

    Hilo la vikalio vya zege kwa upande wangu ni kama mtoto hana mkoba wa shule 'school bag' ukenda kumtafutia 'tool box' iliyo tupu ndio awekee daftari zake, japo itahifadhi, but sio kwa matumizi hayo, inakuwa kama umemkomowa tu. Hapo nadhani nimeeleweka. Sipondi wala kukatisha tamaa, bali ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...