Waziri wa Maji,Mhe. Prof. Jumanne Maghembe akikagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita million 5.5 kwa ajili ya kuhudumia wakazi wapatao 20,000 katika eneo la Itege mjini Dodoma. Tanki hilo ni miongoni mwa matenki manne yanayoendelea kujengwa. Ujenzi wa mradi huu unajengwa kwa ushirikiano wa Serikali za Tanznia na Jamhuri ya Korea kwa gharama ya Sh. Billion 78.
Mkandarasi wa Ujenzi wa Matanki hayo akimuelekeza kitu Waziri wa Maji,Mhe. Prof. Jumanne Maghembe wakati alipofika kukagua ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita million 5.5 kwa ajili ya kuhudumia wakazi wapatao 20,000 katika eneo la Itege mjini Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...