Katibu wa Kikundi cha Muungano kilichopo kijiji cha Oloboloti kata ya Mrijo Halmashauri ya Chemba Mkoani Dodoma kinachojishughulisha na mradi wa kilimo cha nyanya aliyenyoosha mikono katikati Bw Juma Ally akitoa maelezo kwa Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa tatu kutoka kushoto Bi Amina Sanga katika ziara ya kukagua miradi ya Vijana, ziara hiyo ni sehemu ya mafunzo yanayotolewa na Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Mfuko wa Vijana.
Katibu wa Kikundi cha Umoja kinachojishughulisha na mradi wa ufugaji wa mbuzi kilichopo katika kijiji cha Oloboloti katika Halmashauri ya Chemba Mkoani Dodoma Bw. Issa Mwinjo wa kwanza waliosimama mbele akitoa maelezo kwa Afisa wa Idara ya Maendeleo ya Vijana wa tatu kutoka kushoto Bi Amina Sanga katika ziara ya kukagua miradi yaVijana nchini.
Mkurugenzi Msaidizi kitengo cha Mafunzo na Maendeleo ya Ujuzi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Venerose Mtenga akitoa mada katika Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...