Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser akiwaongoza Wakimbizi wazee
kutoka nchini Kongo leo kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao ili watambulike rasmi kuwa ni wakimbizi
katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia za
Wakimbizi 14,000 ikiwa ni sawa na Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimuhoji Mkimbizi kutoka
nchini Burundi, Bibi Karumere (katikati) wakati wa kufanyiwa uhakiki wa taarifa zake ili aweze
kutambulika rasmi kuwa ni Mkimbizi katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani
Kigoma. Zaidi ya familia ya Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa
uhakiki huo kambini hapo.
Mratibu wa Idara ya Wakimbizi Kanda ya Kigoma, Tony Laiser (kulia) akimkabidhi Mkimbizi
kutoka nchini Kongo katika Kambi ya Nyarugusu msaada wa taa inayotumia mionzi ya jua. Taa hiyo
pia ina sehemu ya kuchajia simu za mikononi. Maelfu ya wakimbizi katika Kambi hiyo walipewa
msaada huo leo ulitolewa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR)
kupitia Shirika linalotoa huduma za Kijami na Unyanyasaji wa Kijinsia (IRC) ikiwa ni kawaida
yao kutoa misaada mbalimbali ya kuwasaidia wakimbizi hao waliopo katika kambi hiyo, Wilaya ya
Kasulu mkoani Kigoma.
Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi Nyarugusu, Sospeter Boyo (wapili kushoto) akiwahoji mafundi ujenzi
ambao ni wakimbizi kutoka nchini Kongo, wakati wakilijenga darasa la Shule ya Sekondari Fraternite
iliyopo katika Kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma. Shule hiyo inafundisha
kwa kutumia Mitahala ya Elimu ya nchini Kongo.
Mama Mkimbizi kutoka nchini Kongo akiwa na mwanae, pamoja na wakimbizi wengine wakisubiria
kwenda kufanyiwa uhakiki wa taarifa zao leo ili waweze kutambulika rasmi kuwa ni wakimbizi
katika Kambi ya Nyarugusu, iliyopo Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma. Zaidi ya familia ya
Wakimbizi 14,000 sawa na jumla ya Wakimbizi 68,000 wamefanyiwa uhakiki huo kambini hapo.
Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Jamani, baba mtoto huo si mweusi..nawashauri waliopitia huko wakachukue watoto wao kambini
ReplyDelete