Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel imefungua duka lake la Dodoma kufatia ukarabati uliokuwa
unafanyika wa kuliweka duka hilo kuwa la kisasa zaidi ili kuweza
kuendelea kuwapatia wateja wake huduma bora zaidi.
Uzinduzi wa duka hilo ulifanywa na mkuu wa mkoa wa dodo dkt Rehema
Nchimbi ambapo amewapongeza Airtel kwa mpango kabambe wa kuboresha
maduka yake nchini pamoja na duka la Dodoma.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa
wateja Bi Adriana Lyamba alisema,"Leo tunazindua rasmi duka hili lenye
muundo mpya lililopo katika barabara ya Mkuu hapa Dodoma ikiwa ni moja
kati ya mikakati yetu ya kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma zetu
na kupunguza msururu wa wateja wanaoingia dukani hapa kupata huduma
mbalimbali.
Kwa kupitia duka hili wateja wetu watafurahia huduma zetu
za pesa mkononi za Airtel Money ,internet na kuweza kununua muda wa
maongezi pamoja bidhaa zikiwemo simu za mkononi na vifaa vya huduma za
mawasiliano na huduma nyingine nyingi.
Sasa wateja wetu wanauhakika wa kupata huduma bora kwa haraka zaidi
kupitia duka hili. Tutaendelea kutoa huduma za kibunifu zenye uhakika
na zenye ubora wakati wote kupitia mtandao wetu bora na mpana ulioenea
zaidi nchini. Lengo letu ni kuhakikisha tuwapatia wateja wetu uzoefu
tofauti katika huduma zetu na kufikia matarajio yao. aliongeza Lyamba.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh, Dkt Rehema Nchimbi alisema"
nawapongeza sana Airtel kwa juhudi hizi za kuboresha utoaji wa huduma
za mawasiliano kwa watumiaji nchini. Sote tunatambua mawasiliano ni
nyenzo muhimu katika kuunganisha jamii na kuendesha shughuli za
kibiashara na kiuchumi nachukua fulsa hii kuwaomba wakazi wa Dodoma
watumie vyema nafasi hii kupata huduma bora zitakazorahisisha
uendeshaji wa Shughuli zao mbalimalbali za kila siku".
"Serikali inaunga mkono juhudi zinazofanywa na Airtel na kuwaomba
waendelee kuwekeza zaidi katika kuboresha upatikanaji wa huduma za
mawasilaino nchini. tuko tayari kushirikiana Airtel katika
kuhakikisha tunaweka mazingira bora ya kuendesha biashara ili
kuwawezesha wananchi wetu kufaidika na huduma hizi za mawasiliano na
hatimaye kuwa maisha bora."
Airtel imeendelea kuboresha maduka yake nchini ambapo hivi karibuni
imezindua maduka yake mapya katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha
Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro, Bukoba na
Zanzibar yanategemewa kuzinduliwa kabla ya mwisho wa mwezi huu wa
septemba.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema (kati) akikatata utepe
kuashiria kulizindua rasmi duka la Airtel Dodoma lililopo barabara ya
Mkuu mkoani humo, anaeshuhudia wakwanza kulia ni mkurugenzi wa airtel
huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba na Meneja biashara wa Airtel
Dodoma Bw, Stephen Akyoo wakwanza kushoto, Airtel imefanya uzinduzi wa
duka hilo jana baada ya kuzindua maduka mengine katika mikoa ya Dar
es Salaam, Arusha Mwanza Mbeya na Mtwara. Maduka mengine ya Morogoro,
Bukoba na Zanzibar pia yanatarajiwa kuzindulia mwezi huu.
Meneja mauzo wa Airtel Mkoa wa Dodoma Bw Stephen Akyoo akiwa na wafanyakazi wengine wa Airtel Dodoma akitoa maelezo mafupi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi kuhusiana na muonekano wa duka jipya la Airtel Dodoma lililopo barabara ya Mkuu muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa huyo kuzindua duka hilo jana.
Kati kati ni Mkuuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema nchimbi akiwa na Mkurugenzia wa huduma kwa Mteja Airtel Bi Adriana Lyamba (shoto) na Meneja wa Duka hilo mkoani hapo Bi Elida kulia wakikata keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya uzinduzi wa duka jipya la Airtel mtaa wa Mkuu mjini Dodoma jana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt Rehema Nchimbi akiongea na wananchi na wanahabari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa duka jipya la Airtel mkoani Dodoma barabara ya mkuu Jana, Airtel ilizindua duka hilo kwa dhumuni la kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake nchini.
Wafanyakazi wa Airtel mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Airtel kufungua Duka jipya mkoani hapo mtaa wa Mkuu jana, picha na mpigapicha wetu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...