Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Baraza la Ushindani (FCT) Bw.
Nzinyangwa Mchany akiwaeleza waandishi wa Habari (Hawapo pichani)Kuhusu
majukumu ya Baraza hilo na kutoa wito kwa wananchi kulitumia baraza hilo pale
itakapohitajika kwa madhumuni ya ustawi wa uchumi wa Jamii na Taifa kwa
ujumla.wakati wa Mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa
Sheria wa Baraza hilo Bi. Hafsa Said.
Hassan Silayo MAELEZO.
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Baraza la ushindani limewataka wananchi kulitumia Baraza hili kwa manufaa ya
Taifa na ustawi wa uchumi nchini.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi Nzinyangwa
Mchany wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam.
“Baraza la ushindani lipo kwa ajili ya watu wote hivyo wananchi hawana budi
kulitumia kwa manufaa ya Taifa”. Alisema Nzinyangwa.
Aidha, Nzinyangwa alisema kuwa baraza la ushindani ni chombo maalum cha
rufaa za maamuzi au amri za Tume ya Ushindani na mamlaka za udhibiti kwenye
sekta za Miundombinu,huduma za maji na nishati.
Pia alisema kuwa kesi zinazosikilizwa kwenye baraza zinahakikisha uzingatiaji wa
misingi ya udhibiti ili kuleta umakini katika kusimamia sekta husika na ushindani
wa haki sokoni.
Akizungumzia kuhusu rufaa zilizowahi kusikilizwa na baraza hilo Nzinyangwa
alisema kuwa rufaa zinazosikilizwa na baraza la Ushindani zimegawanyika katika
makundi manne.
Akizitaja rufaa hizo Nzinyangwa alisema ni rufaa kati ya mtoa huduma na
mlaji, hii ni pale mlaji anapopewa huduma mbovu au hafifu kwenye sekta
inayosimamiwa na mdhibiti kama maji, simu, nishati ya umeme pamoja na bidhaa
za mafuta ya nishati.
Pia kuna aina ya rufaa kati ya wauzaji wawili wa bidhaa ya aina moja ama
mbadala wake kama kampuni za usafirisha au kampuni za simu ambapo shauri hili
litapelekwa kwa mdhibiti wa sekta husika na iwapo upande mmoja hautaridhika na
uamuzi unahaki ya kuombea rufaa uamuzi huo kwenye baraza la ushindani.
Akiendelea kutaja Rufaa hizo Nzinyangwa alisema kuwa pia ipo rufaa kati ya
mtoa huduma na mdhibiti wa sekta na hii ni pale mdhibiti wa sekta anapoandaa
utaratibu wa kudhibiti sekta na ikiwa mdau anaona utaratibu huo hautoshelezi
au haukufuata sheria mdau ana haki ya kuwasilisha malalamiko kwenye chombo
kilichotoa uamuzi huo.
Pia mdau wa soko anaweza kukata rufaa kwenye Baraza la ushindani ikiwa tume
ya ushindani imetoa amri kwenye soko au kutunga kanuni Fulani juu ya utaratibu
kuhusu usimamizi wa ushindani kwenye soko ambao mdau anaona uamuzi huo
haukuwa sawa.
Tume ya ushindani ina jukumu la kukataza uzalishaji na uuzaji wa bidhaa bandia
sokoni,katika jukumu hilo maamuzi hayo yanaweza kukatiwa rufaa na mdau
kwenye Baraza la Ushindani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...