BIA ya Kibo
Gold Lager imechaguliwa kuwa mshindi wa medali ya dhahabu kwa ubora duniani
inayotolewa na ‘Monde Selection’. Kibo ilipokea utambulisho huo wa kimataifa
wakati wa sherehe za 53 za kila mwaka zilizofanyika huko Bordeaux, Ufaransa.
‘Monde Selection’
ni tuzo zinazotolewa kila mwaka tangu mwaka 1961, kwa ajili ya bidhaa za
vinywaji na chakula. Huendeshwa na kampuni ya Biashara ijulikanayo kama
‘International Institute for Quality Selections’ ya Brussels, Ubelgiji. Bidhaa
hizo huonjwa na kujaribiwa ili ziweze kupewa alama ya ubora.
Akizungumza
baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti
Breweries Ltd (SBL), Bw. Steve Ganon, alisema: “Kama familia ya SBL,
tumefarijika sana kusikia habari hii kubwa inayoihusu bidhaa yetu, kitu kama
hiki huwa hakitokei hivi hivi; tumekifanya kitokee... Kwa hiyo ninaipongeza
timu nzima ya SBL kwa juhudi zao za kujenga imani kwa watumiaji.”
Bia ya Kibo
Gold ilizinduliwa miaka 15 iliyopita chini ya Kibo Breweries. Kwa bahati mbaya,
bidhaa hiyo haikudumu sana sokoni kutokana na kufungwa kwa kampuni ya Kibo
Breweries. Nembo hiyo ilichukuliwa na Serengeti Breweries Ltd na kuzinduliwa
upya Juni 2012 katika kiwanda cha SBL kilichopo Moshi Brewery ambako ndiko
huzalishwa na kusambazwa sehemukubwa ya kaskazini mwa Tanzania katika mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha, Tanga na Manyara, kati ya mingine mingi.
Lengo la bia
ya Kibo Gold ni kutanua wigo wa vinywaji vya Serengeti Breweries Ltd na
kuwashika watumiaji wa daraja la kati katika soko la kaskazini mwa nchi. Agosti 2013,
Kibo Gold ilibadilishwa na kuwekwa katika chupa yenye shingo ndefu maarufu kama
‘mwanamke nyonga’ ili kwenda na wakati na matakwa ya soko la kisasa.
Sasa Kibo
ipo katika chupa yenye shingo ndefu ya milimita 500 ikiwa na asilima 5.5 ya
kileo inayodumu kwa kipindi cha miezi sita. Kauli mbiu ya Kibo ni ‘Yaone maisha
katika mwanga bora.’Bia hii kwa
sasa inauzwa rejareja kwa Sh 1,800.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...