Bondia maarufu wa kike mwafrika barani ulaya Bintou Yawa Schmill aka "The Voice" anatarajiwa kupanda ulingoni tarehe 26 September 2014, atapambana na bondia  Mirjana Vujic katika ukumbi wa Stadthalle/ Saalbau Frankfurt-Nied, Mjini Frankfurt ujerumani.

Bondia Bintou Yawa Schmill aka "The Voice" mzaliwa wa Togo ambaye anapigia uzito wa Welterweight -64 Kg, urefu mita 1.71  historia yake hapo mwanzo alikuwa bondia wa ngumi za ridhaa kwa muda miaka mitano,kuanzia mwaka 2007 alianza kuingia katika ngumu za kulipwa (professional boxer) amepigana (fights) 8 kashinda 7(wins) kashinda kwa
K.O.s 7.

Bondia Bintou Yawa Schmill ni juzi tu katimiza umri wa miaka 30,mwanafunzi wa chuo kikuu cha Bremen na ndiye aliyelipamba jarida la maarufu la warembo "Penthouse",bondia huyo wa kike anayeiliwakilisha bara Afrika Ughaibuni mara nyingi amefananishwa
na SIMBA (Bintou is the Lioness),Simba ambaye ukimuona mpishe njia ulingoni. Bintou "The Voice" Schmill sasa kapania kuweka rekodi ya kuwachapa wapinzania wake kila kona duniani !
Mengi kuhusu bondia Bintou Schmill aka 'The Voice" usikose at
For more information write to
 Africans support your children and make them proud NOW! http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=iEmjbWJr

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...