Habari zilizotufikia hivi punde zinasema Jeshi la polisi mkoani  Geita limekamata bunduki saba (pichani) na mabomu kadhaa ya machozi eneo la Ushirombo wilaya ya Bukombe ikisadikiwa kuwa ni kati ya bunduki kumi zilizoporwa na majambazi yaliyovamia kituo cha polisi Bukombe na kufanya mauaji ya askari polisi wawili waliokuwa zamu  jana. Bunduki hizo, nne zikiwa SMG na tatu aina ya Shotgun  pamoja na panga zimepatikana  katika tanuri la kuchomea matofali zikiwa zimefichwa pamoja na mabomu hayo.

Habari zinapasha pia kwamba katika msako huo mkali unaoendelea, Jeshi hilo pia limewatia mbaroni watu wawili wanaohisiwa kuwa ni  majambazi yaliyohusika na shabulio hilo, mmoja akiwa kakutwa  akiwa na bomu  juu ya mti, majira ya jioni ya leo. 

Jeshi la polisi nchini tayari limetangaza dau  la shilingi millioni 10 kwa mtu yeyote atakaye fanikisha kuwakamata au kuwabaini waliohusika na vitendo hivyo. Taarifa zaidi tutaendelea kuwaletea kwa kadri zitavyopatikana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...