Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeharibika vibaya baada ya kugongana uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.

Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 86 kujeruhiwa vibaya. Kwa mujibu wa Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.

Hali iliyoipelekea basi hilo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndogo kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 35 kupoteza maisha hapo hapo,wakishuhudia tukio hilo la ajali.


Buldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokoaji ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 33 mpaka sasa

  1. Hii ndio Tanzania yetu na madereva makini kabisa. Mungu awapumzishe kwa amani wote waliofariki na awasamehe dhambi zao. Majeruhi wote wapone haraka kwa msaada wa Mungu Amina

    ReplyDelete
  2. inna lillah wa inna ilayhi rajiun

    ReplyDelete
  3. Poleni! Ajali hizi haziwezi kuisha sababu tanzania hakuna sheria ya kuhukumu madereva pumbavu kama huyu wa j4 express. Viongozi wetu wanalijua hili na ndio maana hata hii watatoa tu rambirambi.

    ReplyDelete
  4. Poleni waliojeruhiwa na kufikwa na msiba baada ya ajali hii ya kutisha. Hatutachoka kusema madereva tuwe waangalifu, muendeshe pole pole mfike, haraka haraka haina baraka.

    ReplyDelete
  5. Mpaka lini? Mpaka lini? watanzania wasio na kosa wataendelea kufa kwa ujinga wa madereva na polisi wanaojali matumbo yao. SERIKALI INAPASWA KUBEBA LAWAMA PIA, hizo wanazoziita highway ni finyu sana, hakuna sehemu ya kupaki magari pembeni au service roads, Juzi niliandika kwenye gazeti kuwa moja ya kazi ambazo rais wetu ataendelea kufanya ni kutoa rambirambi kila siku kama si mara 3 kwa wiki. Tatizo lipo kwa serikali na kwa wananchi wenyewe, serikali mnajenga barabara finyu na chini ya viwango ndiyo maana magari yanapinduka ovyo hata kwenye sehemu ambazo kupinduka ni vigumu kwa sababu ya ujenzi mbovu wa barabara usiozingatia viwango na pia kama ni highway kwanini barabara zisipanuliwe au zijengwe lane mbili mbili kila upande kwa mtindo huo hakutakuwa na ajali kwani anayetaka ku-overtake afanye anavyotaka kwa sababu kuna lane(barabara) mbili zinazokwenda upande mmoja. Polisi wahakikishe sharia zinafuatwa na faini na vifungo virefu vitolewe kwa wale wanaoendesha bila kutii sheria za barabarani na walevi kama wanavyofanya nchi za wenzetu, ni nafuu afungwe dereva na maisha ya watu 35 yaokolewe na kuokoa wengine wasiwe vilema.

    ReplyDelete
  6. very so sad, waokoaji mbona wanakodoa macho tu?

    ReplyDelete
  7. Poleni sana waTanzania mnaozidi kupoteza maisha na viungo kila kukicha!

    Na huu sasa ni mchezo wa kawaida hapa kwetu! Watu wafariki, viongozi watume rambirambi, na kukemea (sijui anakemewa nani!!) mamlaka zifanye uchunguzi, maombolezo yaendelee!!

    Kisa? ni madereva wazembe, barabara mbovu kuitwa highway, magari maobovu, ukijumulisha yote hayo unapata majanga!!

    Watu wanajifanya wanajua kuendesha vya moto na kufanya vitu vya ajabu barabarani!!

    Hivi mamlaka zimeshindwa kudhibiti hili?!

    ReplyDelete
  8. RIP our fellow inocent Tanzanian.Ni jioni hii tukitokea moshi kwenye msiba tumenusurika ajali eneo la tanita kibaha baada ya lori la mchanga kuovatake gari ndogo iliyokuwa ikielekea mlandizi na kuhama kuifuata gari yetu iliyokuwa ikielekea dsm.Sisemi ni jitihada za dereva wetu tu ila mungu alituhurumia mno.Ni kwa neema tu tumesalimika.Asante mungu.

    ReplyDelete
  9. Ajali imetuuma sana lkn kuilaumu tanzania si sahihi maana ajali zinatokea dunia nzima na madereva wazembe wako dunia nzima tuwaombee waFiwa subira katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  10. Abiria nao wanaona gari linakwenda mwendo usio wa kawaida wanajua vifo vinavyotokea kila siku lakini wana kaa kimya ndani ya basi kama dagaa wanasubiri ushahidi kamili wao pia wana takiwa waje juu na kuwa na suti moja ya kumdhibiti dereva na utingo wake kama hawasikii wana uwezo wa kushuka kituo cha karibu na kusubiri usafiri mwingine.
    bora kuchelewa kufika au kutokufika safari uliyokusudia ukarudi ulikotoka kuliko kufariki hivi kwa makusudi ukijua kuwa usalama wako uko hatarini.
    personal responsibility must be taken here.
    hao madereva ndio hawasikii na nyie abiria ndio hamuoni pia.

    ReplyDelete
  11. MIMI NASHANGAA SANA KILA SIKU BARABARA ZINAJENGWA LAKINI NI ZILE ZILE NYEMBMBAMBA KAMA MKIA WA PANYA. LINI TUTAJENGA BARANARA BANA NA HIGHWAY TANZANIA? INASIKITISHA SANA. KILA SIKU MH: RAIS UNAKUJA MAREKANI NA SEHEMU NYINGINE UNAONA MIUNDOMBINU YA WENZETU, KWA NINI TUNAKUWA HATUNA WIVU WA MAENDELEO KAMA YA WENZETU JAMANI? INAUMIZA SANA SANA. ANYWAY, WANAOKUFA SIKU ZOTE HAWANA MAKOSA EE MUNGU UWAPE RAHA YA MILELE. TUMECHOKA KUSIKIA AJALI KILA KUKICHA TANZANIA TANZANIA NO, NO IT IS ENOUGH.

    ReplyDelete
  12. Wenye magari makubwa muwaheshimu wenye magari madogo, bajaji au boda boda. Sasa unaona vifo hivyo vyote. Sasa haraka ilikuwa ya nini? Hivi ungepunguza mwendo na kupita polepole msingefika???

    ReplyDelete
  13. Hayatakwisha, hayatakwisha, hayatakwisha..... Inauma, inahuzunisha na kutia hasira. Miaka yote nimekuwa muoga kusafiri, kwanini? Naogopa AJALI. Si kufa Maana najua iko siku nitakufa. Lakini kuachwa kilema, nisiejiweza kwa lolote naogopa sana Hilo na stipend liwatokee wengine. Sababu tujilaumu wenyewe, tumeshindwa kuiwajibisha serikali yetu kwa majanga yote yanayotukumba. Ni wengi, si ajali tu... MIKATABA MIBOVU, ELIMU MBOVU, UBADHIRIFU ULIOPINDUKIA, RUSHWA ILIYOKITHIRI, HUDUMA ZA JAMII MBOVU NA NK. SIKU TUTAKAYOAMKA NA KUIWAJIBISHA SERIKALI KWA YOTE HAYO NDO SIKU MADHILA YANAYOTUSIBU YATAFIKIA TAMATI YAKE. TUBADILIKENI NDUGU ZANGU.

    ReplyDelete
  14. Hii ni moja ya sababu kubwa ya ajali afrika. Kuwa na barabara za kupishana muda umefika kuziondoa. Najua serikali haina hela ya kupandisha kiwango cha infrastructures lakini wenzetu huku ukiamua kuendesha kwa kasi unahamia lane nyingine ya mwendo kasi.na wale wa pole pole wanabaki upande wao wa kushoto.

    ReplyDelete
  15. Mungu awalaze mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  16. inna lillah wainna ilayhirrajiuun

    ReplyDelete
  17. HUYO ALIYEANDIKA TUSIILAUMU SERIKALI ANA UFINYU WA UWEZO WA KUFIKIRI AU HAELEWI ANACHOONGEA AU HAJAWAHI KUTOKA NJE YA TANZANIA. AELEZE LEO WAPI KUNA AJALI ILIYOUA WATU 35 DUNIANI ZAIDI YA TANZANIA? KWANINI TUSIIGE NCHI ZILIZOENDELEA KWENYE UDHIBITI WA MADEREVA NA KUWATIA ADABU WALE WOTE WANAOFANYA UPUMBAVU NA KUWEKA VIFUNGO VIREFU ILI IWE FUNDISHO KWA WANAOZEMBEA? LEO WAMEKUFA WATANZANIA WASIO NA HATIA 35 NA WENGINE WAMEKUWA MAJERUHI SANA WENGINE WAMEKATIKA MIGUU, UJUE HAO WALIOKATIKA MIGUU, MIKONO AU VIUNGO VINGINE WALIKUWA WAZIMA JANA TU SASA NANI ATAWATUNZA? SERIKALI? MISIKITI AU MAKANISA? SIDHANI KAMA KUNA MMOJA KATI YA HAO ATAWATUNZA? WATABAKIA MASKINI MAISHA YAO YOTE KWA AJILI TU YA SERIKALI (POLISI) KUACHA SEKTA YA USAFIRI IJIONGOZE KIHUNI HUNI NA POLISI WAJICHUKULIE RUSHWA KANA KWAMBA HAWALIPWI. SERIKALI YETU IMELALA SIKU ZOTE NA SIDHANI KAMA ITAAMKA SASA HIVI. KESHO UTAONA KWENYE BLOG HII TAARIFA YA SERIKALI KUWA RAIS AMETUMA RAMBIRAMBI NA AMESIKITISHWA SANA NA WATANZANIA KUFA. HAPO HAWAJAANGALIA UBOVU, UFINYU WA BARABARA NA ULIO CHINI YA VIWANGO, BARABARA ZETU HAZINA WARNING (ILANI) YA KUONYESHA DARAJA AU SEHEMU YA HATARI NA VIWANGO VYA MWENDO UNAOTAKIWA KUENDESHA KWENYE SEHEMU TOFAUTI.
    SIJAWAHI ONA MAGARI YAMEGONGANA NA KUHARIBIKA KIASI HIKI....HIVI HUO MWENDOKASI(SPEED) UMERUHUSIWA NA NANI? POLISI...SERIKALI...SUMATRA AU?
    TUNASUBIRI RAMBIRAMBI KUTOKA KWA RAIS KUTUAMBIA AMESIKITISHWA SANA LAKINI HAKUNA HATUA ZA KUCHUKULIWA KWA SABABU TUMEZOEA KUFANYA KAZI TUNAVYOJUA.....HAKUNA CREATIVITY. BAADA YA WIKI MOJA UTASIKIA AJALI NYINGINE MBEYA, MOSHI, IRINGA AU DODOMA....MTINDO WETU ULE ULE....RAIS AMESIKITISHWA SANA!!! UFUMBUZI------HAKUNA! BAADA YA MUDA NCHI YETU ITAJAA WALEMAVU WALIOPATA AJALI KWA MAKOSA YASIYO YAO.

    ReplyDelete
  18. mdau hapo juu hongera sana kwa kuchambua vizuri na kuondoa huo ujinga wa huyo aliyechangia huko mwanzo akisema tusilaumu serikali

    uliyosema yote ni sahihi .... napenda kuongezea it is about time pia haya magari yalazimishwe kuwa na insurance kubwa .... basi likisababisha ajali ... mmiliki na dereva muhusika wajiandae kulipa kila majeruhi/kifo insurance hata ya 100+ millions .... wakishindwa kifungo cha maisha!....na dereva kama ameua ni kupigwa risasi hadharani mpaka afe

    uone kama watakua wanaendekeza huu uzembe

    pia abiria wakiona dereva anakimbiza gari waruhusiwe kumpa kipigo cha paka mwizi!

    INASIKITISHA SANA ... HAO WALIOFARIKI SI AJABU WALIKUA WANATEGEMEWA SANA NA FAMILIA ZAO .... watu wataishia tu kutoa rambi rambi kwenye blogs na magazeti then wanasahaulika

    ReplyDelete
  19. inaniuma sana pia kama waliotangulia kusema WENZANGU BARABARA ZA TZ HUWA ZIMEJENGWA SIMPLE SIMPLE SANA NO CREATIVITY, HAO MAKANDARASI WA TANROADS SIJUI WALISOMEA WAPI!!

    ReplyDelete
  20. Poleni wafiwaPoleni mlionusurika.Nimesoma comments zote neno moja baada ya jingine hadi machozi yamenilengalenga.Kuna tatizo mahali fulani.Mambo matatu hivi yamejirudiarudia sana:

    1:MADEREVA WENYEWE(Kutofuata sheria)
    2:POLISI WA USALAMA BARABARANI(Rushwa)
    3:MIUNDO MBINU(UFINYU WA BARABARA)

    Na mimi naungana na waliotaja hayo maeneo matatu.Tusibodhibiti maeneo hayo matatu tutaendelea kupoteza familia zetu,ndugu,jamaa na marafiki kila siku.

    David V

    ReplyDelete
  21. Mtoa mada hapo juu amesema ufinyu wa barabara ndo chanzo pekee cha hizi ajali.Mi nakataa kwa sababu mi niko uingereza nashuhudia barabara zao za pembeni ni finyu mno ila madereva wana discipline ya hali ya juu ukiacha hizo motor ways kwani uwezo wetu ndo unatufanya tuwe na hizo finyu.serikali isipotupia macho jukumu la uendeshaji vyuo vya mafunzo ya udereva na kuwa kali sana swara la sheria ya barabarani hii aibu itatutafuna vizazi na vizazi.kuna udhaifu wa kufikiri kwa system zetu.hili swara ni aibu ya serikali yetu.Kumiliki leseni ya gari ni ngumu hapa uingereza kuliko passport.tuna kila uwezo wa kudhibiti leseni za madereva kwani sasa ni electronic.hapa kila kosa linakuwa recorded na makosa mengi yanakuingiza kwenye criminal record na kuzuiwa kukamata usukani kabisa. sasa hao wabunge wasikalie mbili na tatu zisizo na madhara kwa mtanzania.KWANI HADI KUFIKIRI tukamuagize raisi kuulizia wazungu? ajali hizo zina tiba ila uwezo wa kufikiri na rushwa ya mtanzania ndo janga la vifo vya wapendwa wetu.Tumechoka kila siku AJALI.Na serikali ipigwe tu maana tumechoka sasa.watu wanaendesha na viroba njoo uingereza ujaribu drink driving hata kama uko peke yako wanakuchukualia kuwa ni muuaji na unaogopwa kama ukoma.ukikamatwa unakaa kwenye record maisha yako yote kila unapoenda huduma nyingine huwezi pata kabisa.serikali inatuma wabunge dunia nzima kujifunza sijui wanajifunza nini.Tumieni pesa kujifunza sehemu nyeti kama hizi zinazotumaliza.barabara nzuri ila ukiamua kuendesha gari lako unakuwa hauna uhakika hata wa kufika unakoenda.maisha gani hayo.

    ReplyDelete
  22. Hivi sisi watanzania tulikosa nini katika kufikiri? Rwanda kuna barabara mithiri ya nyoka na ni milima kila sehemu.Rushwa iko chini sana kaulizeni kama wana ajali sawa na zetu

    ReplyDelete
  23. Poleni wanafamilia wote waliopoteza ndugu zao na majeruhi, Mungu awatie ngungu na awaponye wale wote waliojeruhiwa na pia awalaze mahali pema peponi wale wote waliopoteza maisha. R.I.P ALL.

    ReplyDelete
  24. Naanza kwa kusema poleni sana ndugu, marafiki mliopoteza watu katika ajali hii, Sisi Watanzania tuna huzunika kwa kupoteza nguvu kazi, pia napenda kutoa lawama kwa Madereva wa Mabasi (mimi ni dereva wa toyota vitz Dar) Madereva wamekuwa hawajifunzi kutokana na makosa ndio maana ajali hizi hujirudia mara kwa mara, tukiangalia ajali hii ya Musoma inaonyesha ni wazi kuwa madereva wa Mabasi yote mawili walikuwa Spidi kubwa huku wakifahamu kwamba mbele kuna daraja jembamba na endapo gari nyingine ikitokea mbele itakuwaje, hawakujiuliza hayo maswali, vitu vingine tunamsingizia Mungu eti ajali imepangwa, kumbe ni Shetani aliyepanga kwa kuwatumia hao madereva Marehemu (Mungu awalaze mahali pema peponi). Serikali yetu pia ni ya kulaumiwa inakuwaje sehemu kama ile ikashindwa kujenga daraja la kupishana daraja linakuwa finyu. Jana Wananchi wa Wazo Tegeta wameandamana mambo haya haya ufinyu wa barabara, lazima tuipigie kelele serikali itekeleze wajibu wake kwa wanannchi. Haya ndio maoni yangu, kama nimekosea nicheki kwenye e-mail emmanuelmgana@yahoo.com

    ReplyDelete
  25. KUNA MSEMO WA KISWAHILI: Ajali haina kinga!!! How dumb!

    ReplyDelete
  26. Mungu awaweke kila mmoja mahala anapostahili.

    ReplyDelete
  27. Sababu hawa madereva hawana elimu ya udereva, reseni zao za kuchakachua

    ReplyDelete
  28. Tz ni kichwa cha mwendawazimu cjui tumerogwa?? inatia hasira sana tatizo ni madereva wazembe kama uyu wa J4 express utaovertk vp wakati unajua kuna daraja kwa mbele. Tatizo si ufinyu wa barabara taizo ni serikali kutofuatilia wanaovunya sheria za raisi kazi yake ni kutoa rambirambi na kusikitishwa na ajali badala ya kuhakikisha sheria zinafuatwa. Inasikitisha sana tusubiri tu rambirambi kutoka kwa raisi kwa mkuu wa mkoa wa mara. Serikali amkeni mmelala sana rushwa tu mungu ibakiri tz. Mungu aziweke mahali pema roho za marehemu wote amem..

    ReplyDelete
  29. Wakenya hawakukosea waliposema BONGOLALA. Mtanzania Leo akisikia uraia pacha anatutumuka kwa kuita time ya "wataalamu" was mambo ya uhamiaji ili kuelewesha umma ni jinsi gani taifa litaathirika iwapo watanzania waliopo ughaibuni wataruhusiwa kuwa watanzania. Swami he wako wapi wataalamu na time za kujadili chanzo, sababu na suluhu LA ajari za barabarani ? Ndugu mtanzania; adui yako siyo mtanzania mwenye uraia pacha au wawekezaji kutoka nje, Bali adui yako ni utamaduni was kukaa kimya kwenye mambo yenye tija kwako mfano uko ndani ya basi na dereva hazingatii sheria-husemi chochote, adui yako no mifumo duni ya afya, elimu na miundo mbinu. Adui yako mkubwa kuliko wrote ni RUSHWA. Mtanzania huna haki za kimsingi ndani ya nchi yako; kwenye vyombo vya dola, mahakamani na hata uraiani Kama huna chochote mfukoni. Ndugu watanzania tukae chino na tufikirie mini in kitu cha muhimu kwetu na tukivalie njuga kuona kinatekelezwa au kinarekebishwa, na ajari za barabarani ni moja ya matatizo yetu makubwa.

    ReplyDelete
  30. RIP wote waliofariki kwenye ajali hiyo mbaya...nimesoma comments zote na nimejikuta natoa machozi. Jana ilikua kwao...kesho ni kwetu. Je nn kifanyike???Mabadiliko yaanze sasa...mabadiliko ni ww na mm. Changes should start with us!!! Wote tulio comment tuwe mwanzo wa mabadiliko. Tutakufa kama kuku mpaka lini?? TUWAWAJIBISHE MADEREVA WAUWAJI, POLISI WAPENDA MATUMBO YAO, NA SERIKALI KIPOFU. Mfano kama upo kwny bus na ukaona Dreva ana mis-behave kwa kuendesha gari utadhani kabeba kuku...tuwe chachu ya kuwakomesha. polisi wala rushwa nao hivyo hvyo, na serikali kipofu nayo hivyo hivyo. Tusiishie ku comment tu then tuache wengine watekeleze...Lets be part of it.

    ReplyDelete
  31. samahani kwqa watakaokelekwa............KIMSINGI MWENDOKASI NI ULE ULE ULIOWEKWA NA MAKAMPUNI YA UTENGENEZAJI WA MAGARI..tukilaumu mwendokasi basi tupande mikokoteni ya punda ili tufike salama na amani..NA BARABARA ZOTE TANZANIA NZIMA ZINA VIASHILIO VYA KILA NAMNA ...kona kali . daraja ..kivuko cha waenda kwa miguu... kivuko cha mifugo ama wanyama pori....KWA KIFUPI NIKIWA KAMA DEREVA WA SIKU NYINGI....NIKWAMBA 100% YA TANZANIA NZIMA ALAMA BARABARANI ZIPO ....SASA BASI TATIZO NININI.......NYINYI AMBAO SIO MADEREVA MNAIBA ALAMA ZA BARABARANI MNAUZA....SREPA.... MNATUSABABISHIA MATATIZO SISI MADEREVA......PILI NIKWAMBA KUNA MADEREVA WAO HUENDESHA MAGARI KWA UZOEFU.....HAWA NDIO HULETA HATARI BARABARANI ..... UZOEFU HULETA HALI YAKUJIAMINI NA KUONDOA HALI YA TAHADHARI....... UDEREVA UNAOKUBARIKA DUNIANI KOTE NI UDEREVA WA TAHADHARI NA SIO UDEREVA WA UZOEFU..... asanteni saana ......ila mungu aliwapenda zaidi (G.d.mwambatata)

    ReplyDelete
  32. Poleni sana wafiwa. R.i.p mliotutangulia. Nashauri tunanze mazungumzo ya kuokoana maisha. Maanya vyombo husika vya usalaama barabarani vipo busy vinashiba maana hadi sasa sidhani wameguswa ya kutoshwa. Tulio wengi tulioguswa tunaomba kuanzia sasa tujiokolee maisha ya wezentu wanaolazimika kupanda basi kila leo na yetu sisi tunapoamua kupanda mabasi. Si tunawajua madereva wazuri tutoe picha zao na makampuni yao watu wajue watapanda basi lipi kwa amani. Aha madereva wabaya pia wajulikane, ikiwa nia pamoja na kampuni na basi lipi na picha zao! Watunza mablog tusaideni wekeni sekta ya usalaama barababarani ilisisi wadau tuweze kuchagua nani wa kumkwepa baadala ya kujiweka hatarani kama ilivyo sasa. Tutaweza kudhibiti madereva wazuri na wabaya ktk jila kijiji, mji na mkoa. Ni zoezi ndefu lakini litaokoa ndugu wengi. Kama umeguswa tusaidiane.

    ReplyDelete
  33. Mimi bwana naifananisha Tanzania sawa sawa na mtu tajiri aliyejipatia mali kishirikina utamkuta ana mali nyiiiingi lakini anavaa vibaya au analala pabaya!!! Tanzania ni tajiri sana ila haina maendeleo, raia wake na viongozi wake wote hamnazo wanakubali kula rushwa na matokeo yake watu wengi wanakufa, ukiangalia magari mengi yaliyo barabarani hayana vigezo ya kuwa barabarani lakini kwa kuonga utayakuta meeeengi mabovu barabarani dah!! yaani wote sisi ni wakinga!! ndio maana nawaambia wanangu tufurahi kila siku maana kwa hizi ajari wanaweza kuwakosa wazazi wao anytime so every moment count on them!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...