Nchini Tanzania, wanawake 7,900
hupoteza maisha kila mwaka wakati wa kujifungua. Zaidi ya asilimia 80 ya vifo
hivi vingeweza kuepukika endapo wahudumu wa afya wenye utaalamu wangetoa huduma kwa wakina mama
wajawazito wakati wa kujifungua.
Kwa
kuamini kuwa hakuna mwanamke anayepaswa kufa wakati wa kujifungua, Shirika la
Amref Health Africa Tanzania kwa kushirikiana na Bank za Barclays na Bank M leo
wametangaza nia ya kuongeza nguvu na juhudi za kutunisha mfuko wa kusaidia mafunzo
ya wakunga kupitia kampeni yake ya Stand up for African Mothers.
Kampeni hiyo
ya kimataifa inalenga katika kuongeza uelewa juu ya mchango unaotolewa na wakunga wenye ujuzi katika
kupunguza vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga.
Kampeni
hii pia inalenga kukusanya fedha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wakunga 15,000 katika
nchi 13 za Afrika, kati yao wakunga 3800
wanatarajiwa kupata mafunzo nchini
Tanzania ifikapo mwaka 2015/2016. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Changia mafunzo ya wakunga , okoa maisha ya
mama na mtoto” kwa kuunga mkono nia hii njema unasaidia kuwapatia mafunzo
wahudumu wa afya walio mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto nchini
Tanzania
![]() |
Mmoja wa mabalozi wapya wawili wa kampeni hiyo Mwasiti Almasi akiongea na waandishi wa habari . |
Nchini Tanzania kampeni hii ilizinduliwa
na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 15 Mei mwaka 2012.
Mke wa
Raisi amekuwa balozi wa kampeni hii akiongoza juhudi za kuwaokoa kina mama wa
kiafrika.
Tunayo furaha pia ya kuwatangaza wanamuziki wa kizazi kipya nchini
Tanzania Banana Zoro na Mwasiti Almasi
ambao wamejitoa katika kushiriki na Amref Health Africa kuelimisha jamii juu ya afya ya mama na mtoto kupitia kampeni
hii ya Stand up for African
Mothers.
Mpaka sasa, fedha zilichongishwa
kupitia kampeni hii zimewezesha kusomesha wakunga 80 kwa kiwango cha cheti;
wakunga 10 wanatarajiwa kuhitimu mwezi wa 11 mwaka huu na 70 wanaingia mwaka wa
pili wa mafunzo yao.
Jumla ya wanafunzi 176 wanaongeza ujuzi kwa kupata
mafunzo ya ukunga kwa njia ya masafa, ili kuongeza elimu kutoka
kiwango cha cheti hadi diploma.
Mafunzo hayo yanaendeshwa kati ka vituo kumi
vilivyo katika mikoa ya Mbeya, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Mwanza, Mara,
Zanzibar and Mtwara. Na kiasi cha fedha kilichopatikana mwaka 2013 kinatarajia
kusaidia wanafunzi 60 watakaoanza masomo yao mwezi wa 10 mwaka huu.
Akiongea katika mkutano na waandishi
wa habari mapema leo Mkurugenzi wa Amref Tanzania Dr. Festus Ilako alisema “Tunatoa mchango wetu katika kulisaidia Taifa kufikia malengo yake ya millennia
(MDGs) yanayohusiana na afya kwa kuboresha huduma za afya na kuchangia katika
kuboresha hali ya sasa ya afya ya uzazi. Mafunzo ya ukunga yatawaongezea ujuzi
wakunga walioko na kufundisha wakunga zaidi ambao baada ya kuhitimu watatoa huduma za afya ya uzazi katika zahanati hivyo kuchangia katika
kupunguza vifo vya kina mama vinavyoweza kuzuilika. Tunatoa rai kwenu kuunga
mkono na kubadilisha maisha ya kina mama”
Tunawashukuru wadhamini wote walio
pamoja nasi katika kufanikisha juhudi hizi. Bank M na Barclays bank wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia
mafunzo ya wakunga kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa. Pia tunatambua mchango mkubwa
uliotolewa na Benki ya Authetic Media Group, BG, Coca Cola Excel Management, FBME,
KPMG, NBC, MICHUZI Blog, Mohan’s LTD, Jaffsher
foundation LTD, Jamii
forums, KCB bank, UCHUMI supermarket, IPP media, Push Mobile, , PWC, Pyramid
Pharma, Southern Sun Hotel, Songas, SERENA Hotels,
Serengeti Breweries, Stanbic Bank and TCRA.
Ombi letu kwa mashirika, makampuni ya
uma na yale ya binafsi, pamoja na watu binafsi ni kuunga mkono jitihada hizi
kwa kudhamini mafunzo ya wakunga (mafunzo ya mkunga mmoja yanagharimu dola
3000). Unaweza kuchangia kwa njia mbali mbali, ikiwa ni pamoja na kupitia
·
Account ya benki National Bank of Commerce (NBC), Corporate
Branch, Akaunti Namba 0111030004548
·
Mpesa Namba 0762
22 33 48
·
Tigo pesa Namba 0716 032 441
·
Airtel money Namba 0685 506306.
Kuhusu Amref
Health Africa.
Amref Health Africa ni Taasisi kongwe
ya afya ya kimataifa
isiyo ya kiserikali , inayotoa mafunzo na huduma za afya kwa zaidi ya nchi 30 barani
Africa. Shirika hili
lilianzishwa mwaka 1957 kama “ AMREF flying Doctors” kwa ajili ya kutoa huduma muhimu za kiafya katika jamii iliyokuwa
katika maeneo magumu kufikiwa.
Kwa sasa , Amref Health Africa inatoa huduma nyingi za afya katika jamii
na hasa kwa kuzingatia wanajamii wahitaji ambao wengi wanaishi katika
maeneo magumu kufikika barani Afrika.
Amref Health Africa imejikita katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa
huduma za afya, mafunzo, mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na
mtoto, UKIMWI, kifua kikuu, malaria, maji safi na usafi wa mazingira, huduma za madaktari bingwa na maabara.
Amref Health Africa inabaki kuwa Taasisi ya mfano na kuaminika
kimataifa kwa kutoa huduma bora
za afya na endelevu kwa miaka 57 toka kuanzishwa kwake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...