Shirika la Majisafi na Majitaka limeanza operesheni kata Maji katika jiji la Dar kufuatia madeni sugu yanayodaiwa wateja kufikia zaidi ya billion 44 zinazowahusisha taasisi mbalimbali za serikali, watumiaji wa majumbani na wafanyabiashara mbalimbali.

Akizungumza na gazeti hili, Ofisa Uhusiano wa Dawasco, Bi Everlasting Lyaro alisema operesheni hiyo inatarajiwa kuanza mapema wiki ijayo na lengo kuu ni kuweza kupata fedha hizo ambazo ni malimbikizo ya muda mrefu.

“operesheni hii itaanza wiki ijayo yaani sept 15 na mteja yeyote mwenye deni sugu na la muda mrefu na asiyekamilisha malipo ya Ankara za nyuma atasitishiwa huduma mara moja na kulazimika kulipa faini” alisema Lyaro.

Aliitaja faini ambayo wahusika watalazimika kulipia baada ya kukatiwa Maji kuwa ni Tsh 50,000 kwa wateja wakubwa na 15,000 kwa wateja wadogo.

“pia majina ya wateja wanaodaiwa na kiwango wanachodaiwa imebandikwa katika ofisi zote za kanda za  Mamlaka hizo hivyo mteja akifika katika ofisi zetu ataona jina lake na kiwango anachodaiwa” aliongeza Lyaro.

“Tumewatumia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) wateja wetu juu ya kuanza kwa operesheni hii hivyo hatutegemei mwananchi kujitokeza tena na kulalamika kuwa ameonewa kwa kutopata taarifa kabla zoezi halijaanza” alisema Lyaro.

Alisema timu ya Dawasco itakuwepo katika maeneo mbalimbali ikipita nyumba kwa nyumba na shirika kwa shirika kusaka wote wanaodaiwa na watalazimika kulipa bili zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wanaodaiwa maji walipe, kwanini wanataka huduma bila kulipa, hawajui kuwa mpaka uletewe maji bombani kuna gharama kubwa ambazo wateja lazim tuchangie?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...