PROMOTER BRITTS EVENT MATATANI MJINI STUTTGART,UJERUMANI
Polisi wamesema mpaka kieleweke, M-Nigeria Roho Juu

Stuttgart,Ujerumani,
Anayejiita promota Biritts Event - inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsha jumla ya hasara ya Euro 300,000(Tsh.600 Million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya jumamosi 30 Augost 2014 baada ya msanii wa NASIB ABDUL AKA DIAMOND PLATINUMZ kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart,ujerumani.
 
Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr.Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa
Sindfingen kwa kukodisha ukumbi huo kwa ajili ya african paty na mkutano sio onyesho la muziki kama alivyofanya,na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 ( T-shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe,kwa promota huyo.
 
Awin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonyesho ya bidhaa siyo muziki.

taarifa za uhakika polisi imelipeleka swala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt)
ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria ambao unamweka roho juu
bwana Awin Williams Akpomiemie - BRITTS EVENTS, Polisi inaendelea 
kumuhoji kwa kujihusika na biashara zingine haramu. 
Wakati huo huo tahasisi mbali mbali na jumuiya za wafrika nchini ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemieza kuwadanganya washabiki na kulivunjia hadhi na sifa bara la Afrika nchini ujerumani ,tahasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Watu wasifikirie euro 300,000 ni kwa ajiri chupa walizorushiana walevi pale hapa! bali labour charge za malipo ya askari waliofika pale walikuwa 17 na magari ya kubeba wagonjwa ndio maana gharama za hasara ni kubwa,ujerumani askari wakija katika tukio kama lile uwa wanakulipisha kwa sababu ukuwapa taarifa mapema kuwa kutakuwa na sherehe
    mmagari ya kubeba majerui nayo pia ulipiwa hakuna cha bure ujerumani

    ReplyDelete
  2. Wenzao FFU katika show zao nyuma ya jukwaa yale magari polisi yakuwaga tayari tayari washabiki wakianza na Polisi wanakinukisha,sasa show ya huyu
    poromota mnigeria kulikoni? mbona kuna ubabaishaji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...