
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd. wadau na wananchi wakijipanga tayari kuanza kampeni ya wiki tatu ya kusafisha maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji iliyozinduliwa rasmi na Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi ikiwa ni awamu ya kwanza kwa mwaka huu kabla ya kuelekea kwenye kata nyingine mbili zilimo ndani ya manispaa ya Ilala wakishirikiana na wananchi.
Na Mwandishi wetu
WILAYA ya Ilala imeanzisha kampeni ya wiki tatu ya usafi katika maeneo yaliyopo katikati ya Jijini la Dar es salaam kwa lengo la kutoa elimu na kuyaweka maeneo hayo safi na salama.
Kampeni hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa juma katika eneo la Kisutu na Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi .
Akizundua kampeni hiyo alisema bila suala la usafi kufanyiwa kazi, wageni wataona kwamba mambo katika Jiji la Dar e s salaam ni hovyo hasa ikizingatiwa kwamba kati ya jiji ndio sebule ya Jiji.
Kampeni hiyo inayosimamiwa na kampuni yenye dhamana ya usafi katika eneo hilo la kati ya Green Waste Pro Limited inashirikisha wananchi kwa lengo la kuwafanya wawe washirika wa usafi kwa kujenga utamaduni wa kuchukia uchafu.
Mkuu huyo wa wilaya pamoja na kushukuru wananchi na wanafunzi wa shule ya Kisutu waliofika katika kampeni aliwataka viongozi kujipanga kuhakikisha kampeni hiyo inakuwa endelevu na yenye mafanikio. Kampeni hiyo inafanyika katika kata ya Kivukoni, Kisutu na Mchafukoge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...