Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tarehe 25/09/2014 alfajiri vimeokotwa vipeperushi maeneo mbalimbali mjini Dodoma vyenye ujumbe ufuatao ONYO – DODOMA SI MAHALI PA KUFUGA WEZI WA FEDHA ZA UMMA. UTAKAYEINGIA BUNGENI KUANZIA KESHO, YATAKAYOKUPATA UTAJUTA.

Kamanda MISIME amesema tumeendelea kupokea taarifa za watu wanaodaiwa kuandaa vipeperushi hivyo na tunafanyia kazi ili tuweze kuwakamata ili washtakiwe kulingana na kosa walilolitenda hasa la kutoa vitisho na kuhamasisha uvunjifu wa amani.

Aidha Kamanda MISIME ameongeza ametoa wito kwa wananchi na wageni wanaofika Dodoma watii sheria bila shuruti.  Kila mmoja ajiepushe kujiingiza kwenye kuhamasisha uvunjifu wa amani, kujiingiza katika mikusanyiko isiyo halali na maandamano ambayo yameshapigwa marufuku na Jeshi la Polisi.  

Atakayekiuka na kujiingiza katika vitendo hivyo vya kiuhalifu atashurutishwa kwa nguvu zote kwa mujibu wa sheria za Nchi na kwa mamlaka iliyopewa Jeshi la Polisi.

Kamanda MISIME ameongeza kuwa wananchi na wageni wapenda amani waendelee na shughuli zao kama kawaida kwani Jeshi La Polisi limejiimarisha ipasavyo kukabiliana na yeyote yule atakayekiuka sheria na maelekezo yaliyotolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mlango wa kuingia kwenye mchakato wa katiba si ulikuwa wazi kwa wote walioalikwa. Waliokuwa na sababu za kutoitikia wito walitumia uhuru wao wa kidemokrasia kufanya hivyo. Kati yao wapo waliorudi kwenye mchakato bila ya kujali wale waliowabeza. Sasa hivi vitisho vinatokea wapi? Au kuna kitu ambacho hatuelezwi.

    ReplyDelete
  2.  
     
    I do not agree with what you have to say, but I'll defend to the death your right to say it.
    Voltaire

    Mimi naamini anaejiita mwanademokrasia wa kweli. ataheshim hii view....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...