Mgodi wa dhahabu wa Geita Gold Mine uliopo mkoani Geita. Mgodi huu ni moja ya makampuni yanayowania tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji.
Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mine katika masuala ya serikali na jamii Bw. Clement Msalangi (mbele kwa mbali) akielezea mafanikio ya mgodi wa Geita Gold Mine katika utoaji wa huduma bora kwa jamii na uwezeshaji kwa timu ya majaji na sektretarieti iliyofanya ziara katika mgodi huo.
Meneja Mahusiano ya Jamii Bw. Manase Ndoloma akisisitiza jambo katika kikao kilichoshirikisha uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine na jopo la majaji na sekretarieti kwa ajili ya kumtafuta mshindi wa Tuzo ya Rais ya Huduma za Jamii na Uwezeshaji iliyotembelea mgodi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...