Na Andrew Chale

MWANAMUZIKI nyota anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki nchini, Juma Mussa ‘Jux’ anayetamba zaidi  na vibao vya ‘Uzuri wako’ na ‘Nitasubiri’, ameachia rasmi wimbo wake mpya wa ‘Sisikii’ katika stesheni mbalimbali za redio.

Akizungumza jijini Dar es Salaam , Jux alisema wimbo huo wa ‘Sisikii’ ameutengeneza kwa Mtayarishaji  Maneke wa AM rekodi, ambao ni zawadi nyingine kwa mashabiki wake wote duniani.
Jux aliwataka kuupokea kwa mikono miwili na wasubiri video ambayo itakuwa ya kiwango cha hali ya juu.

“Septemba 9, nimeachia rasmi wimbo wa ‘Sisikii’ katika redio hapa nchini na wadau wangu waoupokee kwa mikono miwili kama nyimbo nyingine ninazotoa, pia wakae mkao wa kuona video ya wimbo huu muda si mrefu,”alisema Jux.

Awali Jux amekuwa akiwonjesha mashabiki wake kwenye shoo mbalimbali zinazoendelea nchini kupitia ziara za muziki wa Serengeti Fiesta mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...