Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam,Kamishna Suleiman Kova (wa nne kutoka kushoto) amewataka askari wote wa Kanda hiyo kufanya kazi kwa weledi, kuzingatia haki za binadamu, na kufuata maadili ya kazi katika utendaji wao wa kila siku.
Kamishna Kova ameyasema hayo mwanzoni mwa wiki hii wakati akiongea na Maafisa na Wakaguzi wa Polisi katika kikao cha utendaji kilichofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay, Kinondoni, jijini Dar es Salaam na kusisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora kwa wateja kulingana na matarajio ya wananchi.
Aidha Kamishna Kova amesisitiza usiri katika Taarifa zinazoletwa au zinazotolewa na wananchi na kwamba kwa kufanya hivyo kutalifanya Jeshi la Polisi kuaminika kwa wananchi. Akizungumzia suala la rushwa, Kamishina Kova amewaasa askari kutojihusiasha na kupokea rushwa kwani ni adui wa haki na kinyume na maadili ya kazi za Polisi.
Amehimiza ushirikishwaji wa wananchi katika kila hatua hasa katika mashauri mbalimbali ya kesi zao na kutenda kazi kwa uwazi hasa wakati wananchi wanapotakiwa kupata taarifa za mashauri yao au wanapoomba ushauri katika kero zinazowasibu.
Kila Afisa, Mkaguzi na askari lazima afanye kazi kwa bidii na ukakamavu ili mchango wa Jeshi la Polisi uonekane wazi kwa jamii ya watanzania na wageni wanaoingia na kutoka nchini pia wale wanaoishi nchini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...