Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (wa pili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa kampuni ya ushauri ya TPF Basse Sambre baada kukutana nao leo ofisini kwake Brussels. Wa kwanza kulia ni Bwana. Stefan Pousset Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo na wa kwanza kushoto ni Bwana Jerome Bestgen Meneja wa mauzo wa kampuni hiyo. Wa pili kulia ni Bwana Nyamtara Mukome afisa katika Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji. Wawakilshi hao walimweleza Balozi Kamala kwamba wamepata shughuli za kufanya Tanzania na wanatarajia kufungua ofisi zao Tanzania. Balozi Kamala aliwashauri watafute Watanzania wa kushirikiana nao ili kampuni yao iweze kuimarika, kuhimili ushindani katika sekta ya ushauri, kutoa ajira na kusaidia kujenga uchumi wa Tanzania.
Home
Unlabelled
KAMPUNI YA UBELGIJI YA TPF SAMBRE YAANZA KUFANYA KAZI TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...