Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola ambapo aliwasisitiza wananchi hao kushiriki kazi za maendeleo na kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Afya ya jamii.
Umati wa wakazi wa kata ya Mlola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wananchi hao.
 Wazee Maarufu wa kijiji cha Lwandai wakifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara za kujenga na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pia katika mikutano yake ya sasa Katibu Mkuu amekuwa akitoa nafasi kwa wananchi kuhoji maswali ,kutoa maoni au ushauri kuhusu maendeleo yao katika maeneo yao.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lwandai ambapo aliwaambia wawe makini na maneno ya wanasiaa ambao wanahusisha hoja ya katiba mpya na uchaguzi wa mwaka 2015, alisema kuwa kuna watu wana sahau kuwa hiyo siyo ajenda ya wananchi na si makubaliano ya vyama vya siasa .
 Kila kona ya uwanja ilijaza watu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...