Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na leo amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo.2 
Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo leo. 3 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara leo. 5 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...