Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishona nguo kwenye ofisi ya
Veronica Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni,kulia ni Mbunge wa Korogwe
Vijijini Ndugu Stephen Ngonyani ,Katibu Mkuu alikuwa kwenye ziara ya
siku moja katika wilaya ya Korogwe Vijijini ambapo licha ya kukagua
miradi mbali mbali ya ujenzi wa maabara na ofisi za CCM alipata nafasi
ya kuwahutubia wananchi na kuwasikiliza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimuelekeza Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kushona nguo kwenye ofisi ya Veronica
Simba (kushoto) iliyopo Mombo Sokoni.

Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na
Ueneziwakinunua matunda kabla ya kwenda kwenye mkutano wa hadhara
Mombo.
Wananchi wakiwa wamekaa kwa shauku ya kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCm Ndugu Abdulrahan Kinana.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kulia) akiwapungia watu wakati wa
kuwasili kwenye uwanja wa mikutano mjini Mombo akiwa pamoja na Katibu
wa NEC Itikadi Nape Nnauye.
Umati wa wakazi wa Mombo uliojitokeza kwenye Mkutano wa Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
KInana ni hazina ya CCM hili halina ubishi! dah sidhani kama atatokea kama huyu!
ReplyDeleteNimechoka juzi anapekuwa kwenye tope!!!