Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza kikao cha
Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vilivyopigania Ukombozi wa Nchi Kusini
mwa Afrika (FLM). Kushoto kwa Kinana ni Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF
ya Zimbabwe Comrade Didymus Mutasa na anayefuata ni Katibu Mkuu wa ANC
ya Afrika Kusini Comrade Gwede Mantashe. Kulia kwa Kinana aliyevaa
miwani ni Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Comrade Juliao Mateus Paulo
'Dino Matrosse' na anayefuata ni Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia
Comrade Nangolo Mbumba.
Mkutano huo wa siku moja umefanyika leo tarehe 10 Septemba, 2014 Jijini
Johannesburg, Afrika Kusini na ulikuwa na ajenda Kuu ya Ujenzi wa Chuo
cha pamoja cha Vyama kitakachojengwa Ihemi, Iringa Tanzania. Madhumuni
ya Chuo hicho ni kubadilishana uzoefu na kurithisha historia ya Ukombozi
kwa vizazi vijavyo.
(Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...