Maandamano ya CHADEMA Mkoa wa Dodoma yamedhibitiwa kwa Mkoa mzima.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishina Msaidizi wa Polisi EMMANUEL G. LUKULA (ACP) (pichani) amesema katika hilo kuna gari lenye namba za usajili T.792 CAX aina ya Pick up Ford Ranger nyeupe mali ya CHADEMA iliyokuwa ikiendesha na CHRISTOPHER NYAMWINJA, Mweneye miaka 52, Mgogo, Mkristo Mratibu wa CHADEMA Kanda ya magharibi ambapo makazi yake ni TABORA mjini limekamatwa mtaa wa KUU karibu na kituo cha mafuta cha GAPCO jirani na WIMPI RESTAURANT likiwa na watu wengine watatu ambao ni:-

1.     LAURENT S/O MANGWESHI mwenye miaka 36, Mkristo, Msukuma Mkulima wa Wialya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

2.     AGNES D/O STEPHANO mwenye miaka 26, Mhehe, Mkristo Mfanyabiashara Mkazi Ubungo MAziwa Dar es Salaam.

3.     ELISHA S/O DAUDI mwenye miaka 49, Msukuma, Mkristo Fundi umeme Mkazi wa TAbora.

Kamanda LUKULA – ACP amesema gari hilo lilikuwa na bango lenye maandishi “TUNAPINGA UFISADI UNAOFANYWA NA BUNGE LA KATIBA”. Likiwa na maandishi ubavuni mbele na nyuma M4C.

Aidha Kamanda LUKULA – ACP ameongeza kuwa kabla ya kukamatwa kwa gari hilo Polisi walilikimbiza na katika kupita kwenye kona/mtaa watu wawili waliruka kutoka kwenye gari hilo na kukimbia kusikojulikana na bango hilo. Watu waliobaki ndani ya gari hilo ambao ni wanne ndio waliokamatwa.
Askari Polisi wakiwa kwenye zoezi la kuzuia Maandamano ya Chadema Mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Tunataka siasa za kutuletea maendeleo na amani, tujadili hoja kwa uungwana, tunaposhindwa kukubaliana pia tusikubaliane bila shari. Tujifunze kutoka Scotland kuwa na siasa zilizokomaa na kuendeleza demokrasia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...