Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kikao cha Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kichozungumzia masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi la kiume huko New York tarehe 24.9.2014. 
 Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa Namibia muda mfupi kabla ya kuhudhuria mkutano Wake wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ta tezi la kiume (prostate cancer) huko New York tarehe 24.9.2014. Mkutano huo umefadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative ya nchini Nigeria. 
 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Debby Rechler (wa kwanza kulia) akifuatiwa na Yvonne Feinstein ambao ni wafanyakazi wa Tanzania Children Fund wakati wa mkutano wa Wake wa Marais uliofanyika huko New York nchini Marekani tarehe 24.9.2014. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Jill Bishop, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TET Foundation ya Marekani.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera Mama Salma kwa kazi nzuri na pia kwa kujua kuvaaa! Hongera

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...