Mdau Hendrich Nambira au Kenny kama alivyojulikana kwenye mchezo wa kuigiwa wa Mambo hayo katika runinga ITV wakati huo, Alifunga pingu za maisha na mke wake Florence kutoka Visiwani Zanzibar. Harusi ilifanyika katika kanisa la Anglican UMCA, Upanga jijini Dar es Salaam  tarehe 23/08/2014. 

Mama Bishanga na mumewe hawakuweza kuwahi siku ya harusi hiyo iliyopendeza sana na kuhudhuriwa na ndugu wengine wakiwemo wadogo wa mama Bishanga Mack Innocent Hatia na Constancia Innocent Hatia, baba mkubwa mzee John Kamota na shangazi Rehema Kamota, bibi wa Kenny mwalimu Agnes Innocent Hatia na ndugu zetu wengine, pia marafiki na wawakilishi wa wasanii toka Bongo movie. Sherehe ya kukata na shoka ilifanyika Lion Hotel.
Bwana harusi Kenny na mkewe Florence wakiwa pwani Oster Bay mara baada kumeremeta kwao.
Maharusi wakikata keki ya harusi yao
Kaka wa bwana harusi Kilian Kamota na mama yao mdogo Fridah Mchauru wakipiga cheers ya shampein .
Dada wa bwana harusi Sizelina ambae ni mtoto wa kwanza wa mama Bishanga akilisakata rumba kwa raha na furaha tele ya harusi ya mdogo wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...