Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa
akimkaribisha wilayani Monduli Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh.
Masaki Okada wakati alipowasili wilayani humo jana Jumapili Septemba
28,2014 kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo
inayofadhiliwa na nchi hiyo.Balozi huyo aliahidi kusaidia vifaa vya
kisasa katika hospitali mpya ya kisasa inayojengwa wilayani humo.
Meneja
wa Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema (kushoto) akimkaribisha
Balozi wa Japan nchini Tanzania,Mh. Masaki Okada hotelini hapo.Pembeni
kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Monduli,Bw. Twalib
Mbasha.
Balozi
wa Japan nchini,Mh. Masaki Okada (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Twalib Mbasha (kulia) na Meneja wa
Hoteli ya Emanyata mjini Monduli,Bi. Neema alikofikia balozi huyo na
ujumbe wake katika ziara yake ya siku mbili wilayani humo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...