Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakisalimiana na Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo la Sumbawanga (kulia) katika Ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la kiinjili la Kilutheri la mjini Sumbawanga Septemba 21, 2014. Wapili kushoto ni Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (wapili kulia) wakimkabidhi zawadi Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo (wapili kushoto) katika ibada ya kumweka wakfu Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga, Septemba 21, 2014. Kulia ni mke wa Askofu huyo, Tunsume Mwaipopo na kushoto ni Askofu Israel Mwakyolile wa Dayosisi ya Konde.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika ibada ya kumweka wakfu Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo katika Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu (kushoto) wakiwa katika Picha ya pamoja na Askofu wa Dayosisi ya Ziwa Tanganyika, Ambele Mwaipopo na mkewe Tunsume Mwaipopo (kulia) katika katika ibada ya kumsimika Askofu huyo iliyofanyika kwenye Kanisa kuu la Kiinjili la Kilutheri mjini Sumbawanga Septemba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Muumba alivyomuumba Adam na hatimaye Eva alikuwa na lengo la kumuwezesha binaadamu (mke na mume) kukidhi tamaa za kimwili za kimaumbile; hivyo Mwadhama Ambele Mwaipopo kuwa na mke wake katika tukio kubwa na muhimu kama hilo ni jambo sahihi na vyema kigwa na binaadamu wote bila ya kujali madhehebu yao na vyeo na dhamana zao za kimadhehebu, hii ni pamoja na wakatoliki. Binaadamu tubadilike tusipingane na asili yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...