DK SLAA,SALUM MWALIM PAMOJA NA JOHN MNYIKA Uchaguzi ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA leo usiku huu umefikia tamati kwa kamati kuu ya chama hicho kupata viongozi wake wamwisho ambao ni KATIBU MKUU ,NAIBU KATIBU MKUU BARA pamoja na NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR

MATOKEO
KATIBU MKUU --DK WILLBROD SLAA--
NAIBU KATIBU MKUU BARA---JOHN MNYIKA
NAIBU KATIBU MKUU ZANZIBAR--SALUM MWALIM
Viongozi awa waliteuliwa na mwenyekiti wa chama hicho kama katiba inavyosema na hatimaye baraza kuu likawapitisha wote bila kuwapinga
mh JOHN MNYIKA anateuliwa kushika nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini mh ZITTO KABWE ambaye aliondolewa katika nafasi hiyo na kamati kuu ya chama kwa kile ambacho kilisemekana kuvunja katiba ya chama hicho

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni huyu Salum mwalimu wa channel 10 na vodacom. Mbona anahuzuni na ni Mzazibari atakaye iwakilisha CHADEMA Zanzibar?

    ReplyDelete
  2. Hongera viongozi kwa kupatiwa dhamana ya kushika madaraka hayo. Mujitayarishe kukuza diplomasia kwa kushiriki katika siasa zilizosafi zinazoegemea zaidi kujadili hoja na kuendeleza nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...