Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani mara tu alipowasili Ubalozini hapo kukutana na Taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazo Tangaza Utalii wa Tanzania nchini Marekani kwenye Working Lunch iliyokua na maswali na majibu iliyochukua takribani saa 2 na nusu.
 Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka.
Afisa Utalii Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Immaculata Diyamett akifungua kikao
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wadau wa Utalii kwa kuja kukutana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyarandu kwenye Working Lunch iliyofanyika Ijumaa Sept 12, 2014 katika jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. Lazaro Nyalandu akielezea machache kuhusu Tanzania na Utalii wake kabla ya kuanza kipindi cha maswali na majibu.
Waziri wa Maliasili na Utalii. Mhe. Lazaro Nyarandu akiwa katika meza moja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula.
Mhe. Lazaro Nyalandu akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na wadu wa sekta ya Utalii nchini Marekani (Tour Oporator and Airlines) ambao wengi walitaka kujua usalama wa nchi, na kero wanayopata watalii kwa kutozwa ushuru kila wapitapo kwenyea mageti ambayo wamedai kero kubwa kwa Watalii na swala la Ebola wengi wakihofia usalama wao lakini Mhe. Waziri aliyajibu maswali yote kwa ufasaha na ustadi mkubwa.
Picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Endeleeni kuhamasisha watalii waje nchini ili uchumi wetu uendelee kukuzwa na mapato yanayotokana na utalii. Tuboreshe huduma na mikakati yetu ya kuboresha utalii.

    ReplyDelete
  2. Ndio tunahamasisha na kuleta watalii nyumbani, na suala la Uraia wa nchi mbili je?

    ReplyDelete
  3. Mi jamani....Immaculata Diyanett baaash!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...