Taswira hii inayosambaa kila pembe katika mitandao ya jamii na Globu ya Jamii kuipata ndiyo chachu ya mjadala wetu ambao mdau unaombwa kuchangia bila kuchafua hali ya hewa. Ukweli ni kwamba THIS IS TOO MUCH! Ni lazima kifanyike kitu ama lifanyike jambo kukomesha maafa ya kila mara nchini kutokana na ajali za barabarani.
Ajali za barabarani!
 Ninalianza shairi, kwa majonzi ya dhahiri,
Kwa kuwa tena si siri, ajali zimekithiri,
Zaua kwa utitiri, hii sasa ni hatari,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Nianze na madereva, kisha nimvae Kova,
Unapokua dereva, tunahisi umeiva,
Si mambo ya kujilevya, na kuua kina Eva,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Umakini safarini, ndio nyenzo namba wani,
Sheria barabarani, zifuate kwa makini,
Sifa za vibarazani, hazina tija jamani!,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Bosi amekuamini, huyu “suka” ni makini,
Akakupa usukani, na vipesa kibindoni,
Vipi waweka rehani, roho za walio ndani?
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Ukanyagapo pedali, hakikisha unajali,
Roho za watu ni mali, kuzitoa ni muhali,
Japo unaenda mbali, mwendo kasi sio “dili”,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Nanyi wana usalama, sikizeni ‘nayosema,
Njiani mkisimama, fanyeni kazi kwa wema,
Adhabu kali lazima, hata kwa akina mama,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Rushwa nayo siyo njema, enyi wana usalama,
Kazi yenu ya heshima, na jukumu lenye dhima,
Ninawasihi kukoma, myafanyayo ni “noma”,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Na wale wenye magari, hili walitafakari,
Gari zataka vipuri, na madereva mahiri,
Gari mbovu sio nzuri, hata kwa walo hodari,
 Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Naiomba serikali, hasa bwana Magufuli,
Njia zenye kona kali, ziboreshwe tafadhali,
Ziwe pana kweli kweli, tuzipunguze ajali,
Ajali barabarani, ni hasara kwa taifa.

Mwamgongo (Bw.)
Mwenyeji wa Tanga,
12/Septemba/2014

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 98 mpaka sasa

  1. Ni rahisi sana! Mamlaka zinazohusika ziamke kutoka usingizini!!

    Fuatilia jinsi adhabu zilivyokali kwa wenzetu ili uone hapa kwetu wahusika wamelala usingizi wakati binadamu waio na hatia wanapelekwa kama kondoo barabarani! Asilimia zaidi ya 80 ya ajali za hapa kwetu ni za makusudi kabisa!

    Matatizo hapa kwetu ni matatu: usingizi, usingizi na USINGIZI, nukta.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acheni lawama enyi kizazi cha adam mmesahau kuwa kila nafsi itaonja umauti basi jiandaeni kuwa wakati wowote sehemu yoyote umauti utawafikia basi mcheni mola wenu mlezi

      Delete
    2. Sawa, lakini.... Japo utampata kila bindamu lakini si lazima uwe umauti express. Haya matukiyo ni zaidi ya ajabu hakuna asiye shikwa na butwaa, na ndicho kinatotufanya tupige makele. Ni kwa mtazamo huo tu

      Delete
  2. HIYO BARABARA IWE YA KWENDA MWELEKEO MMOJA. BARABARA NYINGINE KAMA HIYO HIYO IJENGWE AMBAYO ITAENDA MWELEKEO MWINGINE. NJIA HII ITAPUNGUZA KUGONGANA KICHWA KWA KICHWA KWA MAGARI.

    JINGINE ELIMU ITOLEWE KWA WADAU, NA KUWAOMBA MADEREVA NA ABIRIA KUWA NA SUBIRA WAWAPO BARABARANI. MWENDOKASI UENDANE NA MIUNDO MBINU ILIYOPO.

    ReplyDelete

  3. 1.Madreva wa mabasi wawe na umri kuanzia miaka 45 na kuendelea
    2.Lesen za madreva wazembe zifungwe wanapopata makosa ya kizembe mara tatu...
    3.Ratiba za Sumatra za mabasi zilekebishwe kuondoa uwezekano wa mabasi kufutana na kukimbizana..
    4.Tatizo la rushwa sijui tufanye nini
    5.Tairi zinazopasuka ovyo TBS wanajibu....
    6.Route ndefu kama ya Dar - Kigoma Madreva wawe wawili..
    7.Public awareness dreva akienda mbio abiria wakatae..

    Ni mawazo yangu tu.

    ReplyDelete
  4. kwanza kabisa! ni kuwaadhibu ma trafick na askari wala rushwa barabarani kwa nguvu zote, na la pili ni vyema kila basi kusafiri na askari wawili wa usalama wa barabarani ambao watakula kiapo iwapo wakigundurika kuchukuwa rushwa wataadhibiwa vikali sana ikiwa ni kutozwa faini kubwa na kifungo cha jela si chini ya miaka 7 vyote kwa pamoja.
    wananchi wanauliwa kama hawana thamani!!! khaaa
    by Nyimbo.

    ReplyDelete
  5. Sylvester, FSeptember 10, 2014

    Ni vema kuwekwa sheria kali ikiwemo kifungo na kunyanganywa leseni pale madereva wanapokiuka sheria na kanini za usalama barabarani. Picha hiyo hapo juu,ni wazi kuwa mabasi yote matatu yanaovertake ni makosa. Traffic police wajifiche na kupiga picha za namna hii hasa sehemu za milimani na kwenye kona kali, zikionesha namba ya gari kisha kupiga simu kituo cha polisi kinachofuata.Mtindo wa polisi kusimama barabarani, madereva hupeana ishara na kupigiana simu kujulishana wahali askari walipo. Picha zitumwe haraka kwenye vituo ili wahusika wachuliwe sheria.

    ReplyDelete
  6. Hawa watu wapigwe risasi hadharani. Wala hakuna haja ya kuwapeleka mahakamani. Uhuru na demokrasia vina miapaka yake. China imejenga nidhamu kwa kutambua hilo.

    ReplyDelete

  7. Kupunguza ajari itabidi tuboreshe miundo mbinu. Ushauri wangu ni kujenga double lane katika barabara zote ambazo ni barabara kuu.
    Highways.Tikifanya hivyo tutapunguza kwa kiasi kikubwa ajari za kugongana uso kwa uso na pia wenye haraka watapata nafasi ya kuweza ku-overtake.

    ReplyDelete
  8. Utafiti ufanyike kuhusu kiini cha ajali hizi je ni madereva kuchoka?, Kuwa na haraka? au kutojua kuendesha? au magari yao kutofanyiwa service? Je shida ni matajiri wao kutotaka kununua vipuli na kuwekeza kwenye magari imara? au barabara zenyewe zilivyokuwa designed kwenye sehemu nyingine dereva anakuwa haoni vizuri? au ni ulevi? Ja alama za bararani, matrafiki wetu je wanafanya kazi kwa weledi na umakini? Sijui idara inayohusika ambayo imekuwa ikifuatilia ajali hii nayo itwambie. Mwaka jana ilitokea ajali ikaua Uswisi wakasema haijawahi kutookea kwa miaka thelathini sisi mwezi huo huo ajali kibao, madereva wetu wana matatizo gani? hawaoni gharama za maisha, majeruhi hospitalini na katika kuchangia ujenzi wa taifa? Ni mjadala unaotakiwa.

    ReplyDelete
  9. Asante sana globu kwa kutuachia huu mwanya kuyaongelea haya mambo ya usalaama. Mpigaji picha asante sana yaani bila kupenda imebidi nitoe mtazamo wangu.
    Bila kujali sababu ya magari makubwa matatu kupishana kwa mkupuo na kwa kutizama picha inaonekana ingweza kutokea ajali mbaya sana barabarani kama ajali ingekuwa imepangwa kutokea.
    Kibaya zaidi upande zote mbili zingedhurika vibaya sana, natamani tungepata maoni ya wasafiri pande zote pamoja na makelele waliopiga ya hofu hiyo. Na kama siyo kelele za kukemea madreva wengi walikuwa wanaomba wasalimike.
    Sasa wahandasi wa barabarani mnaona kosa lolote wa mchoro huo ? Mimi si mhandisi lakini naona madereva wataendelea kulifanya hilo kosa hadi ajali mbaya sana itokee.
    Ukiweza kukuza hiyo picha itaonaekana kama kila dereva alivuka mstari kuelekea upande wa pili inavyotakiwa, tatizo ni haya ni magari makubwa, kuvateki karibu na kilima lazima kungesababisha tatizo kama lilivyokuwa kwenye picha na kufanya kila dreva kuonekana dreva kichaa ....na maanisha wano ovateki.
    Haina hajakuendelea kulichambua zaidi bali kuomba madereva kuwa makini. Magari makubwa kuovateki karibu sana na mlima siyo busara kabisa. Kwa vyovyote magari makubwa kwenye eneo hili lazima yatashawishika kuovataki tu hili halina mjadala ruhusa ya kuovateki ifutwe. Japo nimezungumzia sana magari makubwa najua hili tatizo linaweza kuchangiwa na magari madogo, mbali na hayo sijakugusia upande ule wa mteremko.
    Wano ovateki lazima waje kwa kasi sana ilikuupanda ule mlima, wanokuja upande wa pili bila kuosea watakuwa na wanakuja kwa kasi maana wanaelekea kwenye mteremko. Sasa suluhisho rahisi lisilo la gharama ni kufuta kuovatake eneo hilo na kuweka kutuo traffic cha usalama.
    Traffic signs ziwekwe barabani sitaki kusikia ni gharama maana binadamu anayekufa kwenye ajali thamani yake nikubwa zaidi. Wahusika mnaweza kuondoa hili balaa tena haraka tu kama mnasoma maoni yetu kwenye blogu.
    Madereva wanaopita hiyo njia wapewe nafasi ya kutoa maoni yao kuhusu sehemu kama hizi ambazo zina walazimu wao pamoja na magari yanayobeba mashehena kushindana.
    Kona +mlima+gari kubwa haviendani kabisa. Rekebisheni hili haraka sana! Tuokoe maisha ya wasafiri. Usalaama wa binadamu ndilo lengo kuu. Asanteni.

    ReplyDelete
  10. Wanajamii nimelifikira jumla kuu ni utekelezaji wa sheria za usalaama barabani hazifuatwi ama zinatafsiriwa kimakosa na madereva.
    Trafiki anzeni kufanya kazi yenu acheni kupokea hongo maana.mliowengi mnachangia kutokutekeleza hizi sheria.
    Mnauwezo wakulitatua hili tatizo kama mkitaka. Mimi na pendekeza kuwe na zoezi la kupima kituo kipi cha trafiki hakina ajali ama kimepunguza ajali na kituo kinachofanya vizuri kizawadiwe.
    Tuna mashindano ya kila aina hapa nchini na washindi hupewa zawai ilikuhamasisha washindani wa mwaka unaofuatia. nadhani tunahitaji kuwahamasisha matrafiki wa fanye kazi kwa bidii zaidi na zawadi ziwezakuvutia zaidi masponsa mpo najua mtakubaliana bora hivi kulikoni hongo kila pahala, wakati wowote.
    Mimi naona hongo inachanga kwa sehemu kubwa na uvivu wa matrafiki fulani.
    Laiti mngeelewa kudai hongo ni kuomba kama masikini, msingefanya hivyo. Laiti mngejua kila senti unayoenda mfukoni mwako wewe trafiki moja kila siku ingekuza mfuko wenu wa usalaama kiasi kwamba mngepewa mishahara inayoendana na kazi zenu na haya yote ni kama mungetimiza wajibu wenu.
    Laiti mngefuata sheria watu wasingevunja sheria, nyie mumehalalisha utovu wa nidhamu barabarani hivyo nyie muanze kulirekebisha BILA KUONEA WATU. Kuweni mfano wa sheria kwa kuwa mfano bora.

    ReplyDelete
  11. Sidhani kama dereva mwenye akili timamu angeweza fanya uozo huo. Waajiri angaliene sana watu mnao wakabidhi chombo cha mamilioni,na huduma ambayo inabeba uhai wa mtu.Tusiangalie pesa zaidi kuliko usalama wa abiria.serikali haina uwezo wa kuweka lane nyingine je Tufanyeje kwa sasa? Rushwa ni mpaka tupate Rais ambaye dictator ndio itakma.

    ReplyDelete
  12. only god is all might.

    ReplyDelete
  13. Anonymous unayedai kuwa alama ziwekwe na kwamba wee si mhandisi lakini unaona kuna kosa la design: Inaonekana wee ni mmoja wa hao hao madereva. Na pengine tunawalaumu madereva tu lakini ndivyo wanavyofundishwa kwenye vyuo. Kwamba solid line "msitari ulioungana" maana yake unaruhusiwa ku-overtake!! Ukweli ni kwamba solid line hairuhusu ku-overtake. Dotted line ndio inayoruhusiwa ku-overtake kama iko upande wako. Ndugu yangu, usieneze sumu ya ujinga wako kuwa mistari kwenye picha hiyo inaruhusu ku-overtake. Rudi shuleni ukajielemishe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naomba ukuze picha, utaona dotted line ....in the default picture you can only see the dotted line......

      Delete
  14. Jamani hizi ajali azitaisha bila kushirikiana sisi kwa sisi abiria kwa sababu madereva wanaendesha magari kama vile ni mashindano na pia mkiwa mnakataza dereva apunguze mwendo ndio kama vile mmemchochea. Mi nakumbuka tulikuwa tukitokea Mwanza mwezi wa 7 kidogo sana tungeligogwa na train train linakuja kwa kasi na basi letu kwa kasi ni porini na train kuja kuamaki hili hapa break ilifanya kazi sasa kama break isingefanya kazi na hii msg yangu usingeisoma hakuna cha ajali bahati mbaya ni MADEREVA WENYEWE. Please serikali ichukue sheria kali kwa madereva wazembe tunaisha watanzania jamani.

    ReplyDelete
  15. Madereva wanaofanya makosa haya wafutiwe leseni zao ili wakafanye kazi zingine na siyo hizo za kuuwa watu bila hatia.
    Lakini hilo litawezekana kama baadhi ya polisi wataacha kupokea rushwa na kufanya urafiki na madereva hao wazembe.

    ReplyDelete
  16. 1. Madereva wote wa mabasi ya mikoani kuwakilisha D/L zao ziangaliwe upya na mafunzo yao, na mabosi wao (wenye mabasi) waadhibiwe kwa faini kubwa mno yenye kuwafanya kutoajiri 'mashanta'

    2. Ratiba za mabasi zikaguliwe (checking) kila umbali fulani (i.e Kama basi la Dar - Mwanza) ni lazima lifike sio zaidi ya muda fulani mapema zaidi katika kituo fulani cha katikati na destination.
    3. Kutokana na umbali wa safari kuwa na madereva 2/3 kuhakikisha wanaendesha masaa si zaidi ya 8 kila mmoja kwa safari 1.

    3. Speed cameras ziwepo barabarani zenye uwezo wa kuangalia umbali mrefu (ideally ziwe kwenye nguzo ndefu na hasa sehemu za kona na mlima).

    4. Spot checking za mara kwa mara barabarani kuangalia kama dereva amelewa au kazidisha abiria/mzigo.

    5.Askari kanzu kuwepo ndani ya mabasi na magari madogo barabarani kuangalia nidhamu ya uendeshaji ya madereva
    6. HATUA KALI dhidi ya dereva au askari barabarani atayebainika kuchukua rushwa, na kutolewa 'nishai' kwenye vyombo vya habari ili iwe mfano kwa wengine.
    7. ABIRIA WASIWE 'NAIVE' kumkemea dereva mara wanapoona basi linaenda kwa mwendo mkali au dereva anakiuka masharti ya speed ya barabara au uendeshashi mbovu.
    8. Mabasi na malori yawe yanafanyiwa spot checking na askari wa barabarani kama yana ubora wa kuwa barabarani na kama hayana ubora basi wenye mabasi wachukuliwe hatua kali.


    9. WAHUSIKA kupewa vyenzo na ACTION PLANS kuweza kuchunguzwa ni kazi gani wanayoifanya kuweza kupunguza ajali hizo ambazo ni za kizembe mno na kupoteza maisha ya binaadam wengi bila sababu.

    10. Elimu kwa madereva na abiria kuh ajali barabarani na mengi mengine muhimu ambayo sijaandika hapo juu.

    IT IS NOT A ROCKECT SCIENCE AND IT DOESN'T TAKE A PhD TO SORT THE PROBLEM OUT. WHAT CAN WE DO IF WE CAN@T SORT OUT SUCH A SIMPLE PROBLEM WHICH COSTS OUR BELOVED ONES LIVES???? DO WE NEED WAWEKEZAJI PIA?

    ReplyDelete
  17. 1. Kila dereva lazima wa bus lazima achukue kozi na kushinda mtihani kabla ya kupatiwa leseni.
    2. Mabus yawe yanakaguliwa mara kwa mara, kama vile breki, tairi na hata madereva wake.
    3. Wamiliki wa mabus lazima wanunue liability insuranace kabla hawajaruhusiwa kufanya biashara hiyo. Kama kuna ajali watu walipwe kutoka kwenye hiyo insurance na kama haitoshi basi wafirisiwe. Hii itawafanya wenye mabus kuchagua vyema wafanyakazi wao.
    4. Kwa vile mamlaka imeshindwa kazi basi wananchi wawe wanachukua hatua pale inapoonekana kama dereva anaendesha vibaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Naunga point no.3. Safi sana...
      .

      Delete
  18. 1. Madereva wote wa mabasi ya mikoani kuwakilisha D/L zao ziangaliwe upya na mafunzo yao, na mabosi wao (wenye mabasi) waadhibiwe kwa faini kubwa mno yenye kuwafanya kutoajiri 'mashanta'

    2. Ratiba za mabasi zikaguliwe (checking) kila umbali fulani (i.e Kama basi la Dar - Mwanza) ni lazima lifike sio zaidi ya muda fulani mapema zaidi katika kituo fulani cha katikati na destination.
    3. Kutokana na umbali wa safari kuwa na madereva 2/3 kuhakikisha wanaendesha masaa si zaidi ya 8 kila mmoja kwa safari 1.

    3. Speed cameras ziwepo barabarani zenye uwezo wa kuangalia umbali mrefu (ideally ziwe kwenye nguzo ndefu na hasa sehemu za kona na mlima).

    4. Spot checking za mara kwa mara barabarani kuangalia kama dereva amelewa au kazidisha abiria/mzigo.

    5.Askari kanzu kuwepo ndani ya mabasi na magari madogo barabarani kuangalia nidhamu ya uendeshaji ya madereva
    6. HATUA KALI dhidi ya dereva au askari barabarani atayebainika kuchukua rushwa, na kutolewa 'nishai' kwenye vyombo vya habari ili iwe mfano kwa wengine.
    7. ABIRIA WASIWE 'NAIVE' kumkemea dereva mara wanapoona basi linaenda kwa mwendo mkali au dereva anakiuka masharti ya speed ya barabara au uendeshashi mbovu.
    8. Mabasi na malori yawe yanafanyiwa spot checking na askari wa barabarani kama yana ubora wa kuwa barabarani na kama hayana ubora basi wenye mabasi wachukuliwe hatua kali.


    9. WAHUSIKA kupewa vyenzo na ACTION PLANS kuweza kuchunguzwa ni kazi gani wanayoifanya kuweza kupunguza ajali hizo ambazo ni za kizembe mno na kupoteza maisha ya binaadam wengi bila sababu.

    10. Elimu kwa madereva na abiria kuh ajali barabarani na mengi mengine muhimu ambayo sijaandika hapo juu.

    IT IS NOT A ROCKECT SCIENCE AND IT DOESN'T TAKE A PhD TO SORT THE PROBLEM OUT. WHAT CAN WE DO IF WE CAN@T SORT OUT SUCH A SIMPLEST PROBLEM???? DO WE NEED WAWEKEZAJI PIA?

    ReplyDelete
  19. KITU CHA KWANZA KUANZA NACHO NI KWA HAO WENYE HAYO MAGARI YANAYOONEKANA HAPO KUTAFUTWA NA CHERIA KUCHUKUA MKONDO WAKE KWANZA KWA MADEREVA HUSIKA NA MAKAMPUNI HUSIKA.

    PILI BILA KUMUNGUNYA MANENO TUJIPANGE NA ASKARI WETU WA USALAMA BARA BARANI KWANI NI CHANZO NUMBER MOJA KWA AJALI HIZO WANAKUWA NA MAZOEA MNO NA HAO MADEREVA WAMEKUWA ATM ZAO NARUDIA ATM ZAO...WAKIFIKA NI KUPUNGA TU MKONO NA WANAJUA JINSI WANAVYOPEANA, TRAFIC WAO TATIZO VIGALI VIDOGO NA MAROLI.

    KINGINE NI SWALA ZIMA LA USALAMA WA UBORA WA MAGARI HUSIKA MATAIRI NA UBORA STICKA WANAUZIWA BILA KUKAGULIWA MAGARI....IGP CHUKUA HATUA BADILISHA HAO TRAFIC WAENDE KULINDA BANK NA HAO WENGINE WAJE BARARANI KWA MAELELKEZO MAALUM....WASIZOEE KAZI MOJA CCP MOSHI NA KWINGINEKO HAKUNA ANAYESOMEA UTRAFFIC....

    VIFO N VINGI JAMANI TUONEENI HURUMA....

    ULEVI KWA MADEREVA NA UZEMBE WOTE UNARUDI KWA WASIMAMIAJI AMBAO NI ASKARI IGP PITA COUNTER ZA POLISI USIKU WENGI AMA WOTE WANAKUWA WAMELEWA ,,,JARIBU PALE CENTRAL NA KWINGINEKO UTAONA ...

    ReplyDelete
  20. Kampuni ya basi bila kujalisha nani dereva likikutikana na makosa matatu katika mwaka mmoja basi mabasi yao yote yatabidi yawe na Road Marshal kwenda na kurudi, kwa muda wa miezi mitatu, costs zote zibebwe na mwenye basi

    ReplyDelete
  21. MAGARI YOTE MAKUBWA NIKIWA NA MAANA MABASI NA MALORI,YAWEKEWE CHOMBO KINACHOITWA "SPEED LIMITER" KWA MAANA BASI SHERIA IKIWEKWA KWAMBA MABASI/MALORI SPEED MWISHO 80/KM,BASI NI HAPOHAPO DEREVA HAWEZI ZIDISHA.
    KUWEZESHA HILO ZOEZI KWAMBA HUWEZI PATA LESENI YA BIASHARA BILA GARI YAKO KUWA NA HICHO CHOMBO,KWA WALE WALIOKUWA NA LESENI BASI WAHITAJIKE KUJAZA FOMU UOYA ZA MAOMBI.
    NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA NDIO MFUMO WALIONAO.
    HII ITASAIDIA KWA KIASI KIKUBWA KUPUNGUZA AJALI,PAMOJA NA MENGINEO YALIOTAJWA HAPO AWALI.

    "INAUMA NA KUSIKITISHA SANA"

    ReplyDelete
  22. Ama kweli ukisoma haya maoni ndio unajua kumbe matatizo yetu bado yapo kwenye ubongo. Mi sioni la kujadili wala la kuundia tume. Kama mnaweza kuchoma moto wezi kabla hata polish hawajafika! Hawa madereva hapa mnawashindwaje! Tatizo litaisha maramoja

    ReplyDelete
  23. Inatisha hii.
    Wataka kujiuliza jee hawa madreva wanawazimu ama wamelewa.I have a crazy idea Saa nyingine a mad man may save the day.Hawa madreva lack discipline, so think what is the best way to instil pure discipline into them? Answer, the army.Simple then, no one should get a licence to drive a bus unless he has six months military training.Sounds crazy but could work.

    ReplyDelete
  24. Madereva wote wa PSV wapewe elimu kuhusu usalama Barabarani na wae na leseni maalum za kuendesha mabasi na sheria kali zitolewe kama kwenda jela na kunyanganywa leseni.
    Hao maderevva watatu wa mabasi hawjui wafanyalo

    ReplyDelete
  25. Taswira hii inatosha kuwafikisha mahakamani madereva hawa wa mabasi

    ReplyDelete
  26. Enact laws that would allow owners to be sued for billions at civilian courts, that will make owners very strictly to the drivers, beside loosing his job and licence, the bus owner will be liable for hiring unqualified driver, and he has to pay the damage, and in no ways he could come back with a different company name

    ReplyDelete
  27. A) DOUBLE LANE-HAKUNA DAWA KABAMBE KAMA YA KUJENGE DOUBLE LANE.
    KWA KUWA SASA WAMESHAJITAHIDI KUWEKA BARABARA ZA LAMI NCHINI PHASE INA YOUFUATA SASA KWA BARABARA ZA MASAFA MAREFU MFANO:
    1)DAR-ZAMBIA = DOUBLE LANE
    2)DAR- ARUSHA-NAMANGA =DOUBLE LANE
    3)DAR-DODOMA-SINGIDA-TABORA-MWANZA-BUKOBA-MUSOMA =DOUBLE LANE
    HII NAKWAMBIA ITAKATA SAANA MZIZI WA FITINA.

    B) HIGHWAY PATROL POLICE NA ADHABU KALI FOR SPEEDING- KUWE NA HIGHWAY PATROL & WELL EQUIPED Sio wale wanaokula pozi kichakani na kuibuka bali wale wenye Cruisers ambazo zinaenda na trafiki ili kuscan speed za magari katika high way.
    Serika ifanye testing ya approach hii halafu wai-adopt ikionesha strong improvements.

    ReplyDelete
  28. TWILA KAMBANGWASeptember 10, 2014

    Nachangia kdg tu, nadhani pia chanzo kingine matajiri jinsi wanvyohimiza wafanyakazi wao wawaletee kipato, inalazimika waende mbio kufikisha mzigo wa bwana, napia wasafiri wenyewe si watu wakulalamika kwa madereva wanaasiri ya nidhamu ya uwoga hawawezi kukemea maovu!!

    ReplyDelete
  29. Nakubaliana na Mdau kule juu pamoja na kutoa adhabu kali,Mamlaka husika zinabidi kuboresha miundo mbinu Mfano highway za wenzetu zina lane mbili mpaka Lane tatu kulingana na uwezo wa gari kwa lugha ya kiingereza Horsepower HP:
    Mfano
    Lane ya kwanza 0 to 100 HP
    Lane ya pili 100 to 200 HP
    Lane ya tatu More than 300 HP speed zaidi ya 130km/h
    Mdau Berlin.

    ReplyDelete
  30. Haina maana kutoa maoni maana tunaoumia ni wananchi viongozi usafiri wao ni magari yao binafsi na ndege, hawaoni sababu ya kushughulikia hili na wala hawaguswi. Ajali kama kuchinja kuku hotelini lakini hakuna lililotamkwa toka serikalini. Tufe tu tuna maana gani ya kuishi

    ReplyDelete
  31. Kuna mdau anon kasema ukikuza picha utaona kabla a double lina kuna dotted line hata mimi nimeiona. Hata hivyo swala la common sense lina apply kwa wale drivers.....kweli hii ni action item ya kuchukuliwa hatua na kurekebishwa mara moja. Hoja zimewekwa wazi tuone sasa kama hatua itachukuliwa!

    ReplyDelete
  32. Mdau na wa hapo juu nakubaliana na wewe kwa karne hii ya sasa HIGHWAY hauwezi ukakuta ina lane moja iyo ni hatari sana,kwa tanzania japo wangelijaribu basi highway ziwe na Lane mbili nafkiri pia tungechangia kupunguza ajali kwasababu mwenye haraka atakuwa na Lane yake ya kukimbia.pia na Adhabu kali zitolewe kwa madereva wazembe.

    ReplyDelete
  33. ALL SAID ABOVE - WAHUSIKA WANASOMA AU WANAONA NI UPUUZI TU ULIOANDIKWA HAPO JUU??? I BET (SOME) DON'T CARE.WHO IS IN CHARGE OF THE ROAD TRAFFIC SECTION? ACT NOW!!!!!!! BEFORE WE HEAR YET ANOTHER DISASTER.

    MICHUZI TAF HAKIKISHA TRAIL HII YA MAONI INAKAA HAPO JUU KWENYE BLOG MPAKA MCHAKATO UANZISHWE NA TUONE MAFANIKIO YAKE - IKIWEZEKANA IWAKILISHE MEZANI KWAO NA KAMATI HUSIKA ZA BUNGE ZIHUSIKE - SI KILA SIKU KUTANGULIZA RAMBIRAMBI TU (INAUMA) BILA KUCHUKUA HATUA - AFTER ALL HII NDIO MAANA YA KUWA NA BLOG KAMA HIZI - SO BE PROUD KUWA BLOG YAKO INALETA MABADILIKO YA MATOKEO MUHIMU YANAYOWAKERA NA KUWAGUSA JAMII - SI BLOGS ZA UMBEA TU KUTWA NZIMA.(By Mdau aliyeandika points 1-10 above)

    MWISHO - PETITION? AU HAKUNA KITU KAMA HICHO BONGO? WADAU TUSILALE.

    ReplyDelete
  34. Sisi Watanzania hatufuati sheria na speed. sijui watau wanakuwa na haraka ya kwenda wapi? Utakuta kwenye hii barabara mtu anaovertake au kuhama wakati huo mstari wa moja kwa moja bila vistari vya kuachana HAURUHUSU ku-overtake/kuhama,ajali kwei zitaisha?? sheria za barabarani ni muhimu. vibao vinaovyoonyesha alama ni kama urembo kwetu.Tujifunze kwa wenzetu. Na pia watu wakiendesha magari huku wamelewa kweli tunategemea nini??

    ReplyDelete
  35. 1.Madereva wote wa mabasi ya abiria na malori ya mizigo yanayovuka mpaka wa mkoa na mkoa katika safari zake wawe na leseni halali,umri wa miaka kati ya 45 na 55, ndoa halali zilizothibitishwa na vyombo husika, watoto walau mmoja aliyethibitishwa kisheria,na mahusiano mazuri ya kifamilia na familia zao.Hii itamfanya dereva awe na kitu cha kupoteza kama akiuawa katika ajali aliyoisababisha kwa uzembe wake au akinyang'anywa leseni au kupewa adhabu kali kwa uzembe wake.Akiwa na shule ya walau kidato cha nne au cha sita na kozi yoyote ile licha ya kozi ya udereva pia itasaidia. Yaani kazi ya udereva isiwe kimbilio la wakosefu. Mtu akikosa udaktari, uanasheria, ualimu, uinjinia, uandishi wa habari ndio aende udereva- hapana. Udereva uwe ni kazi yenye hadhi yake na miiko yako na vyeo vyake. Vyeo vya udereva visitegemee tu aina ya leseni viangalie pia mambo mengine. Driving should be a profession by its own sake na madereva wawe na vyombo vyao vya kudhibiti profession ya udereva wasijiunge tu kudai haki zao waaangalie pia mienendo yao na waweze kupandishana vyeo na hadhi kwa mfumo wao kama ilivyo kwa madaktari, walimu wa vyuo vikuu, na kada nyingine.
    2. Ili kupata madereva wa aina hiyo inabidi kuwepo na centralized system ya kuajiri na kufukuza madereva wa vyombo hivi. Ikiwezekana kuwepo na public -private partnership kwa maana ya serikali kusimamia ajira na matajiri kumiliki vyombo vya usafiri na kuwajibika kwa malipo na maslahi ya madereva hawa. Matajiri wengi wanaajiri madereva wasio na sifa kwakuwa hawawalipi maslahi ya kutosha.
    3. Jamii ieleweshwe kuwa safari ni gharama. Unapoamua kufanya safari lazima uwe tayari kuigharimia. Si kila safari inatakiwa uende na kurudi siku hiyohiyo na si kila safari unatakiwa ufike siku hiyohiyo na kufanya kazi. Hii itapunguza kiherehere cha baadhi ya wasafiri ambao huwa wanawapagaisha madereva na kuwafanya wakimbize gari wakati mwingine bila ridhaa yao ili kuwaridhisha wateja maana usipokimbia wasafiri hawatapanda tena gari lako. Kazi ya gari sio kumwahisha msafiri mahali fulani kazi yake ni kumfikisha salama msafiri mahali fulani. Ukiwa na haraka funga safari siku moja kabla, lala guest, kula hotelini, kesho endelea na kazi zako.Ndio maana kuna guest house, hoteli nk nk ni kwaajili ya wageni walio katika shughuli nje ya maeneo ya nyumbani kwao. Watanzania wengi wanafikiri kulala guest na kula hoteli ni luxury- sio kweli.

    ReplyDelete
  36. kama alivyosema mdau mmoja hapo juu picha inatoa ufumbuzi wa muda mrefu wa tatizo la hizi ajali, motorways! Barabara za kuunganisha mikoa ziwe lane mbili kwenda mbili kurudi. Zina gharama nishati huko kusini ilipie hiyo gharama.

    ReplyDelete
  37. Haya ni maoni yangu:
    1.Kosa lolote la dereva lazima lirekodiwe kwenye leseni yake.
    Makosa makubwa yakiwa matatu ,leseni ifungiwe mpaka huyo dereva arudi tena darasani kujifunza.
    Na dereva akiomba kazi ni lazima alete/ record ya leseni yake kutoka idara husika.
    Makosa yote ya uhalifu(elevi ukiwa unaendesha,nk) pia yarekodiwe kwenye leseni ili kuwaweka madereva kwenye hali ya umakini.
    Udereva ni kama kazi nyingine ile,lazima dereva aheshimu kazi yake.
    2.Insurance za magari inabidi ziwe na uwezo wa kulipia majeruhi wote gharama za hospital na gharama zote pindi ajali ikitokea.
    Abiria wajue haki yao kudai insurance pindi wamepata ajali.
    Hii italeta umakini wa wenye magari kuajili madereva makini.
    3.Wanasheria wawe makini kudai hizi haki za wanachi pindi ajali zimetokea na ikiwezekani hata kama kumsilisi mwenye gari lisilo na bima ili kulipia gharama za majeruhi na vifo.
    4.Polisi wa barabarani wawe mstari wa mbele kutimiza wajibu wao bila rushwa.Na ikiwezekana kila askari apewe 10% ya malipo ya gari alilokamata.
    5.Miundombinu ya kuwa na barabara za kuenda na ya kurudi ziwe mbalimbali.Ila hili linahitaji pesa zaidi.

    ReplyDelete
  38. Sasa kama kuna lane 1 ndio u-overtake kwenye eneo kama hilo? Inaonekana vichaa kwenye jamii yetu ni wengi na Watanzania tutaendelea kuuwawa katika magari haya. Kuna watu wanatetea ujinga wa kwenye hiyo picha eti kwa vile kuna lane 1! What a stupid argument! Inaonekana hao madereva kwenye hiyo picha pia wameweka comments zao hapa.

    ReplyDelete
  39. 1. dual carriageway with central reservation
    2. Reduction in speed limit
    3. Effective traffic law enforcement

    ReplyDelete
  40. RUSHWA! RUSHWA! RUSHWA!

    Mkiweza kufuta rushwa kwa askari barabarani (traffic), futa rushwa kwenye mamlaka ya leseni, ongeza mafunzo nakufuatilia wavunja sheria ajali zitapungua sana kama sio kwisha.

    ReplyDelete
  41. 1.Nakubaliana na umri wa chini kuwa miaka 45 lakini pia umri wa juu uwe miaka 65 usizidi hapo.NA wawe na mke wa NDOA na ndoa hiyo ithibitishwe na vyombo husika.
    2.Nakubaliana na adhabu lakini adhabu iwekwe ili kukomesha uvunjifu wa sheria sio kama chanzo cha mapato ya serikali.Mara nyingi tunaelezwa jinsi adhabu za barabarani zilivyochangia pato la serikali badala ya kueleza jinsi lilivyochangia kupungua kwa uvunjifu wa sheria za barabarani.
    3. Kuwepo na data base ya serikali ya madereva weledi ambapo waajiri watakuwa wanapeleka nafasi za kazi na serikali kuwapelekea madereva ambao baada ya kuwafanyia usaili watawaajiri.
    4. Kuwepo na chombo cha kiutawala cha kuongoza udereva kama fani ya weledi (professional carrier) kama vile wahasibu, mainjinia,madaktari,walimu na walimu wa vyuo vikuu na madereva wapande vyeo na kuongezwa mishahara kutokana na umahiri na weledi wao sio tu leseni aliyo nayo.
    5. Kila mwajiri mwenye mabasi au malori ya masafa awe na reserve list ya madereva ambao wapo standby ili dereva atakaekuwa katika hali sio nzuri kiakili au kisaikolojia safari yake ichukuliwe na dereva wa akiba mara moja!Madereva wa akiba wawepo katika sehemu mbalimbali ili hatua dhidi ya dereva asiyefuata maadili zichukuliwe mara moja. Madereva hao wa akiba sio lazima wawe kijiweni wakingojea mwenzao ashindwe - hapana - wawepo tu katika shughuli zao za udereva kwa kuajiriwa na watu au kampuni nyingine na hata serikali lakini ikitokea dharura maitwe mara moja na kumnyang'anya usukani dereva mzembe.
    6.Abiria waelimishwe kuwa kazi ya basi ni kumfikisha abiria salama katika kituo anachodhamiria kufika. Kazi ya basi sio KUMFANYA MTU AWAHI KUFIKA. Kama mtu ana shaka na kuwahi au kuchelewa -asafiri siku moja kabla, alale guest, ale hotelini ili siku inayofuata aamkie hapo tayari kwa kazi zake.

    ReplyDelete
  42. neno moja RAISI KIKWETE aningilie nhili tatizo. Kama Kagame anaweza kuiweka sawa Rwanda Kikwete ana uwezo zaidi yake. Mjerumani alikuwa ana chap viboko na ndivyo mwaafrika alivyozoea. Hata msemaje bila mgtu kuchapwa kiboko hakuna atakayeshika aabu na kuheshimu sheria. RAISI aingilie!!!!

    ReplyDelete
  43. from now on ....Ikitokea ajali na abiria waliobaki hai wawajibishwe ...sababu nao wanaona si kama hawaoni...Wangekuwa wanalalamika woote dereva asingefanya hivi...Ila wanakaa kimya matokeo yake ni ajali..then baadae ikishatokea wanaanza kusema dereva alikuwa anakimbiza gari

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haswa! Abiria tukimfahamu dreva kichwa maji hatupandi basi. Tuna goma! Nadhani lazima tuone picha za dreva atakaetunendesha. Siyo kama tunasafiri bure. Abiria tuna haki ya kusafiri salaama. Hebu fikiria, ni kama mtu tunalipia kufa. Cha !

      Delete
  44. Hapo wote mmeongea naona mnazunguka tu...cha umuhimu n kuwafilisi mafisadi wote hela zetu walotuibia na wanazoendelea kutuibia ili tujenge miundo mbinu ya barabara vizuri mnawalaumu madereva bila sbb wanajitaidi sana kuzuia ajali....ila ss hatulioni hilo tunapiga kelele tu zszo na mpango...tembeeni muone kina kiwete,rosam,edward,kineno,na wengne wengi walivotumia mabilions ya umma kuwekeza nchi ambazo zmeshaendelea....wana majumba ya hatari huko ulaya,dubai na America nyie mmekaa mnakazania kulaumu madereva wkt kuna watu wanazopesa za kujenga barabara wamewapa waarab na wazungu wawashikie...inauma sana...wenzangu tulio ughaibuni tusirudi shamba la bibi tukae huku mpaka kieleweke

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usemalo lina ukweli na tunayosema pia ni ya ukweli. Kikubwa hapa ni watu wanakufa wakiwa safarini. Wakati mwingine ni dereva, wakati mwingine ni dereva na chombo chake na wakati mwingine ni anayemiliki, dreva na chombo kibovu......na naweza kuendelea. Kama binadamu ninae jali maisha ya usalaama LAZIMA nipige kelele. Tukipiga kelele watu walio lala nao watapiga kelele tukiwa wengi tunapiga kelele LAZIMA HATUA ZITACHUKULIWA. We stayed too quiet too long and now see the mess our country is in. Tuungane tulibadilishe hili wimbi!

      Delete
  45. Usisahaulike upimaji wa macho kwa madereva mara kwa mara.

    Miwani iwe ni lazima kwa watakaobainika kuwa na uoni hafifu.

    ReplyDelete
  46. 1. Basi ambalo litahusika kwenye ajali, kampuni yake ifungiwe kwa muda wa miezi mitatu (siku 90)isifanye kazi katika pande yote ya nchi kwa muda huo, kwa mfano ile ajali ya Musoma kampuni ya J4 na Mwanza Coach let say yanafungiwa kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu nchi nzima

    2. Kwa wamiliki ambao magari yao yatahusika kny ajali itungwe sheria ili wamiliki wagharamie mazishi, wagharamie huduma muhimu kama elimu na afya kwa wategemezi wa marehemu mpk hapo hao wategemezi(watoto) watapoweza kujitegemea
    pia wagharamie gharama zote za matibabu na vifaa tiba kwa majeruhi mpk watakapopona, vilevile wawahudumie daima wale watakaopata ulemavu wa kudumu

    HII ITASAIDIA SANA KUPUNGUZA WALAU ASILIMIA SABINI YA AJALI ZINAZOTOKANA NA UZEMBE WA MADEREVA NA UBOVU WA MAGARI.. LENGO KUU NI UWAJIBIKAJI..

    3. Waziri wa uchukuzi, waziri wa miundombinu na waziri wa mambo ya ndani, mna kazi kubwa ili kufit kny wizara zenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hatupo serious basi kama liloanguka juzi ukiliona ni mkweche kabisa mpaka stelingi inachomoka wahusika wanafanya nini kila siku wanaliona lipo barabarani na safari ndefu ya tabora -dar tunategemea nini?dereva anaovatek magari kibao bila tahadhari. Wahusika tuache kukaa kwenye hamsini na kupata buku mbili mbili tufanye kazi.abiria tuache kushabikia mambio yasiyo ya msingi tumwambie dereva acha kukimbia kwa ushirikiano wa abiria wote ni haki yetu kufika salama.nchi za wenzetu trafiki akikamata basi bovu anapewa cammission so inawapa moral tuanze na hapa nyumbani pia itasaidia pia.

      Delete
    2. Naliunga wazo lako!

      Delete
  47. barabara nne mbili kwenda mbili kurudi....hakuna solution nyingine

    ReplyDelete
  48. mimi nipotofauti kidogo na wenzangu,tutawalaumu madereve wawatu bureeee,JAMANI WAKRISTO NA WAISLAM WOTE TUNA MWAMINI MUNG,JAMANI AJALI NI MPANGO WA SHETANI,TUSALI SANA KILA MARA KUMLILIA MUNGU ATUEPUSHE NA MWOVU SHETANI,YEYE NDIYE CHANZO,ANATAFUTA DAMU ZA WATU,TUZIFUNIKE BABARABA KWA MAOMBI TU.

    ReplyDelete
  49. Baada ya kuons ajali ngingine kwenye link nyingine imenilazimu kuuliza. Haya mabasi mbona yanapondeka vibaya sana wakati wa ajali ? Inaleta picha kama vile tuna low standards za magari makubwa.
    So far issues si nyingi na ufumbuzi wa kuyatatua yapo na haya hitaji tume, na mengine hayana gharama.
    Wizara husika wajibika. Bana traffic na wamiliki wa magari whether ni makubwa au madogo.
    Abiria jihudumie kwa maana kwamba wengi mna simu toeni taarifa ofisi za mabasi ticketi zingine zinakuwa na number ya kupiga. Toeni taarifa polisi inapowezekana. Tumeni ripoti kwenye mitandao ya simu na blogu na walio kwenye mabasi mengine mkiona dreva kichaa pigeni picha kama inawezekana. Tuwajue!!! Mmiliki asipo mshughulikia dreva mhalifu au trafiki akiendelea kumfungia jicho hakika itatokea namna tutawaondoa barabarani hawa dreva kicha, tena kihalali.
    Tumechoka! Tumechoka!
    Madreva wazuri mnawajua hawa madreva washenzi watajeni, amatudokeze muda wao wanao endesha wengine bado hatuja amua kufa barabarani.

    ReplyDelete
  50. hizo basi zote zifungwe CCTV kwamba ajali ikitokea dereva atakuwa responsible moja kwa moja bila kupinga.

    ReplyDelete
  51. Yaan ss watanzania sijui niwaambie vp ili muelewe...tuwapigie kelele hao mafisadi tuingie barabarani kwa maandamano ya amani kushinikiza mafisadi warudshe pesa tujenge barabara mbili kwenda mbili kurudi tuone kama kutakua na ajali nyingi kiasi hiki...hamna cha ulev wala umri...tatizo barabara ndogo...alaf m nashangaa waziri husika na waziri mkuu kwann hawajiuzulu kwa vifo vya ndg zetu....m siwapendi viongozi wa bongo...hzo hospital zenyewe za kutibu majeruhi hamna...wa mama wajawazito wanalala chini temeke hospital eti mbunge mtemfu ananunua cd anaacha kuchangisha vitanda na magodoro...hapo temeke n mjini sa je maneromango inakuaje si ndo mama wazalia ndani....aibu sana kuongozwa na watu wapumbavu kama hawa tulio nao hata wakija huku nje hamna wanachoongea cha mana wanabana pua tu rudini nyumban...tuje kuvunjika viuno na barabara zenu mbovu...

    ReplyDelete
  52. Binafsi nilifanya machache yafuatayo ili niwezekujua chanzo cha ajali barabarani husasan kwa mabasi ya abiria

    1.Nilipofanya utafiti kupitia jeshi la polisi,SUMATRA na takwimu za hospitali, nikaelewa kuwa chanzo kikubwa cha ajali za barabarani kisababishi kikuu ni madereva kwa asilimia ipatayo 78%-80% asilimia nyingine 22%-20% nisababu nje ya dereva zikiwemo hali ya hewa, barabara,ubovu wa magari n.k

    2.Niligundua kuwa mabasi yaliyo sajiliwa na kupewa leseni za PSV yapo zaidi ya elfu 60 na hivyo kufanya wastani wa zaidi ya abiria Mill3 husafiri kwa mabasi nchi nzima kutoka sehemu moja kwenda nyingine kila siku ,na kufanya idadi ya abiria kwa wastani wasiopungua Million 2.5 kuwa katika hatari ya ajali na athari zake.

    NINI chakufanya??? hiki ndicho nilichokifanya http://kariakootz.com/new-music-dereva-makini-banaba-amini-dayna-mr-blue/ na hii http://kariakootz.com/video-mtayarishaji-c9-aandaa-wimbo-wa-dereva-makini-ukiwahusisha-wasanii-wakubwa-nchini

    ReplyDelete
    Replies
    1. Safi sana tuhitaji wadadisi wengi zaidi kama wewe. Karibu kila mtu ameona kwa sasa tatizo linaloongoza ni madereva kuendesha magari vibaya, recklessly, then kama ulivyotaja kuna sababu nyingine. Asante kwa link na maoni yako.

      Delete
  53. Kwanza kabisa maereva waliokuwa wanaendesha magari haya wanyang'anywe leseni for life.Means wasekae waendeshe gari yeyote Tanzania, then itakuwa fundisho kwa madereva wengine kuwa atakayefanya hivyo amesalimisha leseni yake permanently.

    ReplyDelete
  54. Mawaziri wa Usalama wa Raia na Uchukuzi na Mawasiliano walnyeshe mfano.

    ReplyDelete
  55. Kumwomba Mungu atuepushe na roho ya mauti iliyoingia nchini. Mungu ndo kila kitu

    ReplyDelete
  56. Dawa yake ni Police wawewana patrol hizo highway mara wakiona hivyo msimamishe dereva hapahapo anfunguliwa mashitaka 2 selikali ijaribu kufunga camera za patrol wakiona wanamsimamisha anayangawa Driving licence kazi hiyo itawapa fundisho pia uanpelekwa mahakamani kosa la uzembe barabarani hiyo ndio dawa yake muafaka

    ReplyDelete
  57. Wabongo mnachobishia hapo ni nini hasa? Picha imeonyesha vizuri sana na barabara inaonekana vizuri mno. Mnaosema zijengwe double lane unadhani tatizo la ajali ni kwa sababu ya single lane? Ukiangalia hiyo picha madreva wameovertake mabasi hayo kwenye kona, na pia space form one bus to another is like zero which means hata ingekuwa double lane kwa jinsi mabus hayo yalivyoongozana ni wazi yatagongana tu.Kinachoonekana hapo ni speed walio nayo, na pia kukosa ufahamu kuwa hapo ni kwenye kona hawezi kuona gari zijazo mbele.Kitu kingine ni hiyo mistari imewatahadharisha vema kabisa.

    Tatizo la madreva wetu hawajui thamani ya watu waliowabeba, na pia watu waliobebwa pia hawajifahamu thamani yao,kwa sababu wote wanaona vioja vinavyofanywa na hao madreva lakini wamefumbia macho. Kuna mdau mmoja hapo juu amesema kitu cha maana kuwa kama wananchi wanaweza kuwaadhibu vibaka au wezi kwa kuwachoma moto kwa kosa la kuiba kuku au baiskeli iweje wakose ushirikiano wa kumwadhibu dreva anayehatarisha uhai wao kiuzembe hivyo?

    Jamani abiria ndio wenye majukumu ya kumwadhibisha dreva anayechezea maisha yao kiutaniutani namna hiyo.Mbona wanafunzi wanagoma mashuleni na vyuoni wasipotendewa haki fulani, iweje abiria ambao wanajua kabisa uhai wao uko hatarini na ni mtu mmoja anahatarisha washindwe kumwadhibisha? Mimi ni mpitaji sana wa njia hiyo hapo ni milima ya uzdizungwa ni kishangao kikubwa sana kwamba madreva wanaweza kuovertake sehemu za kona namna hiyo tena bila haya na hata kujali.

    ReplyDelete
  58. Tatizo ni tamaa ya madereva, we utakuta mtu anakomaa et anaendesha bas Dar-Kampala, Kampala-Dar mtu mmoja bila kupumzika, mwisho wake dereva anachoka anasahau kuwa yupo
    kwenye usukani

    Kitu kingine wadereva wetu hawajasoma, mtu anajifunzia kwenye gari la Noah, baada ya siku mbili unakuta ni dereva Dar-Bukoba,

    kilichopo ni serikali kuwa makini na wadereva ambao hawajaenda shule na wale wanaovuta madawa,

    Mfano kuna chuo cha taifa cha usafirishaji (NIT) wanatoa elimu juu ya usafirishaji na elimu kwa madereva, ni muhimu sana hao madereva wetu wakapite huko kwanza ndo wapewe Driving licence C

    ReplyDelete
  59. Hawa madereva tatizo ni kutojua alama na sheria za barabarani.
    Ni madereva wangapi wanajua maana ya mstari uliounganika katikati barabarani una maana gani?

    ReplyDelete
  60. 1.Nakubaliana na hoja ya kuboresha miundombinu lakini miundombinu ni msaada tu. Lengo ni kupunguza ajali zinazoweza kuzuilika. Kuzuia ajali kunahitaji zaidi weledi na commitment ya madereva kuliko ubora wa barabara. Zipo ajali zinazotokea katika eneo la barabara zuri ajabu!
    2.Nakubaliana na wazo la adhabu kali. Sheria na adhabu zinasaidia saaana, lakini tusisahau ZAWADI. Kuna madereva wameendesha hayo magari tangu ujana wao hadi ubabu bila kuvunja springi ya gari hata mara moja achilia mbali ajali- Je jamii/serikali inawatambua watu hawa?Inawapa zawadi gani? Kuwepo kwa data base ya madereva na chombo cha udereva ni muhimu sana ili kufuatilia utendaji kazi na halki za madereva bila kujali ameajiriwa na kampuni binafsi au serikali.
    3. Tufike mahali tutofautishe udereva na umiliki wa gari. Si kila mmiliki wa gari anastahili au ana sifa ya kuwa dereva kama vile ambavyo si kila mmiliki wa shamba anastahili kuwa afisa ugani, si kila mmiliki wa hoteli anastahili kuwa mhotelia, si kila mmiliki wa shule anastahili kuwa mwalimu nk nk
    4.Tufike mahali tukubali kuwa udereva ni kazi, is a profession just like ualimu, uafisa ugani,uhotelia,nk nk. Mtu asiingie kwenye udereva kwakuwa ameshindwa kuingia katika nyanja nyingine zoote- hapana.Udereva sio kazi ya watu wasio na uwezo wa kufikiri ni kazi inayohitaji uwezo mkubwa saaaana wa kufikiri na kutenda tendo sahihi mara moja maana shida ni kwamba hakuna fursa ya kufuta even the slightest error made by a driving driver. Udereva sio sawa na kuandika kwa kompyuta ambapo ukikosea kuna nafasi ya "delete"- there is no deletion in driving. We need smart people to take smart decision in order to avoid accidents. Tukikubali kuwa udereva is a profession- itatusaidia sana kupunguza ajali lakini tukiendelea na mawazo ya "mpeleke VETA akajifunze walau udereva" as a last option baada ya kushindikana kotekote ajali zitaendelea.
    4. Ifike mahali madereva wajue kuwa gari ni gari tu hata iwe ndogo inastahili heshima zote za gari. Madereva wengi wa malori na mabasi wanasababisha ajali kwa kudharau gari ndogo au aina fulani ya gari kwahiyo hawataki kuendesha nyuma ya gari ambayo wanaidharau na wapo radhi kuipita hata kama sehemu ya barabara haiuruhusu kufanya hivyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimefurahi point no.4, na nakubaliana nalo. Natamani haya maoni yangefika bungeni....

      Delete
  61. Mawasiliano kati ya madereva ajali nyingi zinatokana na kutojua nini mbeleni kwao

    ReplyDelete
  62. hatua za kuendesha uingereza.

    1.Kama dereva mpya unapatiwa provisional licence ili ujifunze gari na kupewa mkataba wenye masharti ya matumizi

    2.Unapewa provisional ili upate mafunzo stahiki na hapo hapo ama kabla unatakiwa ujifue kwa vitabu na dvd za mafunzo ya theory. theory imesheheni mambo yote yanayohusu usalama-alama,documents,insurance, kukabiliana na vikwazo (hazards)nk

    3.Baada ya kujiridhisha unaweza kubook theory test amabyo inasimamiwa na mamlaka ya udereva DSA.Test ina maswali hamsini na kama sikosei inabidi upate 45/50 na test haina uchakachuaji kwani iko online na iko centralized.

    4.Ukipass unapewa cheti chako ila si mwisho wa safari kwani lazima uanze kujiandaa na practical test.instructors wanakuwa monitored na DSA na inabidi wakupitishe viwango vinavyostahili kutokana na syllabus ilivyo.ukishaiva unaweza kubook practical test nayo ambayo ni kiama kwani wao ni kama majudge huwezi kupass kiujanja ujanja kwani lazima udemonstrate viwango vya udereva. unaendesha kwa mfano round about kupita speed tofauti tofauti kukagua gari nk. ukionyesha unaweza unapewa cheti na leseni yako.



    Adhabu.

    mfano wa adhabu.

    1. kuendesha na lerner bila kuwa na msimamizi unapata point 3 na unapigwa faini mahakamani na point unakaa nazo miaka minne.ukikamatwa mara ya pili adhabu inazidi

    2.kuendesha umekunywa unaweza kufungwa ,faini ama vyote na unaingia kwenye criminal record ya maisha serikali na jamii inakuchukulia kama muuaji.

    4.bila insurance- mahakamani, faini kifungo na criminal record
    criminal record nchi hii ni doa kubwa sana kwani kuna mambo mengine huwezi fanya kama baadhi ya kazi ama kupatiwa passport

    kwetu Tanzania.
    -kila mmoja anajua leseni alivyoipata.hivyo vyuo vyetu vinashirikiana na mamlaka kwa kutoa leseni za rushwa.miaka hiyo niliingia barabarani siku nne nikalipishwa pesa leseni ikaletwa ina kila kitu,ukianzia saini za traffic na stamp duty.

    -ulizeni madreva wengi wamezipataje hapo mjini.

    -juzi juzi ubadirishaji wa leseni TRA walopanga foleni pale ngozi wanakumbuka kuwa hatukuwa tunaulizwa pindi ukiweka 5000 tu katikati ya leseni kumkabidhi askali na aliandaliwa mtu pembeni wa kukusanya hizo pesa. na zoezi lilikuwa chini ya mamlaka tofauti.

    -ni magari mangapi hayapati ukaguzi

    -madereva wangapi wanaendsha wakiwa wamelewa, wanaumwa magonjwa yasiyoruhusu uendeshaji kama macho kisukari kifafa nk.

    cha kufanya

    1.Vyuo vyote na mamlaka za kusimamia udereva zisimamiwe na serikali na kama binafsi serikali iweke masharti magumu na iyasimamie.

    2.Insurance companies zitungiwe sheria na zishikiane kwa mfano hapa nikifanya kosa kwenye insurance company A nikikimbilia B nakuta naye ni kama A Tu ana information zangu hivyo kama inapanda kwa A kwa B ni vile vile.

    3.Serikali iamke wawe wakali katika masuala yanayohusu maisha ya mtanzania.isiwe tu pole inatosha wawe na nia ya dhati kutafuta dawa ya matatizo.

    4.Magari yote yakaguliwe kila mwaka na kupewa certificate kwa mfano hapa uingereza inaitwa MOT certificate ukiingia tu barabarani hata kama ni siku moja baada ya kuexpire system inaanza kukutafuta.

    5.mkonga utusaidie leseni zote ziwe kwenye system.dereva akikamatwa kigoma askali apate kuona driving history yake.na kama mtu kazuwiwa kuendesha basi sysytem ionyeshe nchi nzima.

    6.uanzishwe utaratibu wa kuweka record ya criminal record ya watanzania wote kwenye database ili tunapotaka huduma kama kazi,uraisi,ubunge nk tuwajuwe watu whahalifu kwani ndo wanaoendeleza mchezo wa rushwa serikalini.

    7.Raisi ajae aje na nia ya ku crack down RUSHWA-Rwanda wameweza hatuhitaji mzungu atupe mbinu ya kupambana na Rushwa ambayo inamaliza hiki kizazi.

    Mwisho nimshukuru mkuu wa wilaya Michuzi kwa page hii niwaombe tu radhi kama nimeandika kwa makosa kwani nilikuwa na haraka na sikupata muda wa ku proof read.

    God bless Michuzi ,God bless Tanzania






    ReplyDelete
  63. Ndugu wananchi, tuanze na kujiuliza maswali kabla ya kuanza kulaumu upande wowote.Ile ajali iliyotokea kule Musoma ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso na SUV kusukumwa kwenye mto, unafikili ingetokea kama barabara ya kwenda ingekuwa na lane mbili na ya kurudi lane mbili na huku zingetenganishwa na vyuma hasa eneo la daraja? Haya mabasi yasingepata nafasi ya kugongana. Kitu kingine kinacho ongeza ajali barabarani ni madereva wasiokuwa na nidhamu barabarani,wasio kuwa na elimu ya kutosha, wajeuri na wasio sikiliza wenzao. Serikali nayo inatakiwa kuliangalia upya hili tatizo la ajali za magari mara kwa mara.Kuna ajali zingine kama dereva kamkwepa mbuzi, kumbe ni jinni au mambo ya uchawi. Sina muda wa kutoa mawazo yangu mengi hapa lakini nataka kusema yapo mambo mengi yanayosababisha ajali barabarani sio tu uzembe wa polisi au madereva. Hali ya umasikini inaturudisha nyuma pia, tunaendelea kutumia vibarabara vidogo kwa shida, kama utajiri upo kwanini tusipanue mabarabara tukawa na lanes more than two ingesaidia kupunguza ajali. Aksanteni!

    ReplyDelete
  64. Tatizo na Viroba vinachangia plus bangi...Unakuta dereva anaendesha gari Wa mabasi ya Mkoani pia Daladala ye bila kustua kidogo anaona kama hatokuwa fiti...Hivyo akistua akiwa njiani anakuwa hajali tena...Si mizigo tuu / Uzito uwe unapimwa pia madereva wawe wanakaguliwa kama wametumia kilevi chochote wakati wa kuanza safari na huko kati kati ya safari baada ya km fulani..

    ReplyDelete
  65. tatizo kubwa la ajali ni miundo mbinu, niko kwenye nchi flani ya asia unatembea thousands of kilometers barabara ikiwa imetenganishwa upande mmoja na mwengine kwa hiyo hizi ajali za uso kwa uso hazipo, ila kwa barabara za namna hii unategemea dereva atoke Dar mpaka Mwanza bila ya ku overtake haiwezekani

    ReplyDelete
  66. lemnge ombeniSeptember 12, 2014

    maoni yangu ni kama

    1.wawepo wakaguzi professional kukagua mabasi kabla ya kufanya safari.trafiki wanakagua ila hawana taaluma hiyo wanachek tu tairi na kujali rushwa huku maelfu wanapoteza maisha

    2.sio kila ajali ni uzembe wa madereva nadhani uzembe mkubwa upo kwa wakaguzi wanaokaa maofisini tu(sumatra)na wamiliki pia wanazembea kufanya servise za mabasi yao

    3.kuwe na chama cha madereva chenye nguvu.dereva awe manager kwenye basi na nguvu ya maamuzi.awe na mamlaka ya kuzuia safari kama anaona basi halina vigezo au lina hitilafu.kwa sasa madereva hawana power yoyote kwani akigoma anafukuzwa kazi na anapewa mwingine

    4.madereva wawili kwa safari ndefu.mwanza/kigoma,mbeya,kahama musoma nk kutokea dar na pia wapitie course ya(psv)public service driving programme

    ReplyDelete
  67. Abiria ndiyo Jibu sahihi za ajali. abiria wasipande basi ambazo zina madereva ovyo wasiojali maisha yao. Mbona Scacandinavia waliweza, makampuni haya lazima yaige mfano wa mabasi ya Scandinavia. NI UZEMBE TU WA WAMILIKI WA MABASI, mimi ningekuwa na mabasi kama haya madereva wangu ningewajua mwenyewe. mwendo kasi mwiko, uzembe huna kazi, malalamiko kutoka kwa abiria huna kazi. mkataba wa kazi miaka miwili ukifanya vizuri mkataba unapewa mwingine n.k

    ReplyDelete
  68. 1.Lane zilizotenganishwa ni muhimu na tunaposema lane si lazima ziwe na lami. Hii itajenga tabia ya kuwa na mipango ya lane zilizotenganishwa kila tunapofikiria kujenga barabara.
    2. Kuimarisha mafunzo ni muhimu lakini mafunzo ni gharama ili gharama hizo ziweze kupata uhalali kuna umuhimu wa kupitia upya mfumo wa ajira na maslahi ya madereva ili watu waweze kuwekeza katika elimu ya udereva.
    3. Kuzuia rushwa ni muhimu lakini hilo sio la traffic police tu ni letu sote wanajamii. Na kwa kiasi kikubwa jamii inachangia. Mtumishi wa serikali akistaafu na kuishi maisha ya kawaida anaonekana lofa ila yule mwizi mwizi akistaafu akiwa na mali kibao zisizoeleweka amezipataje ndio anonekana yupo safi. Utasikia "hela imeliwa na wajanja" yaanii mwizi jamii inamwita mjanja.Kwa namna hiyo polisi wa barabarani nao inabidi waibe hapohapo barabarani maana nao ni wanajamii.Ni swa tu na muuza mkaa wa barabarani anavyojaza chenga za mkaa katikati ya gunia na kuweka mkaa mzuri juu ya gunia ili kumwibia mteja, muuza maziwa anavyoongeza maji katika maziwa ili kumwibia mnywaji, mwanafunzi anavyoibia mtihani ili kuiba haki ya yule mwenye kutumia uwezo wake halali wa akili, nk nk KUHUSU RUSHWA hili ni la wote wala sio la serikali wala la nani ni watu wote- jamii inahitaji kufanyiwa overhaul ya kimaadili. Serikali ina mchango wake katika kutunga sheria kali dhidi ya rushwa na kusimamia utekelezaji wake lakini jamii isipobadilika hata uweke sheria kali vipi.

    ReplyDelete
  69. 1.pamoja na mikakati yote yaanzishwe makampuni makubwa yenye kuendesha usafirishaji. Tuachane na hao ma investors utakuta mtu Ana basi moja tu .serikali ianzishe kampuni kubwa ambazo watu watanunua hisa

    2.drink driving iangaliwe kwa jicho la ziada

    3. Jamii tuanze kampeni ya kupiga rushwa baada ya serikali kuonyesha udhaifu wa kuikabili

    4.serikali ianze mkakati wa kuinvest katika two lane

    5.madreva wa abiria waanzishiwe programme ya elimu na wawe kuanza kidato cha nne

    6.chama cha madereva kiwepo na kiwe na katiba ma alum iliyoenda shule

    7 ukaguzi wa Magari , insurance viangaliwe upya

    ReplyDelete
  70. Kama wakubwa wanaoendesha nchi wanakula rushwa, je unataka askari trafic yeye rushwa yake ale wapi? Siku wakubwa wataacha kula rushwa na askari trafic wataacha rushwa na ajali zitapungua. Na mambo mengine mengi yatarekebika nchini. Chanzo cha matatizo yote ni rushwa iliyoshamiri kule juu kwa wale wanaoendesha nchi, kwa maana wengine wote kutoka kule juu mpaka chini kabisa lazima na wao watafute mahali pa kula. Rushwa is a killer.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sikubaliani na mtazamo wako wa,rushwa kwa sababu siyo kitu halali never mind nani anakula rushwa. Nakubali ipo ktk chanzo cha matatizo mengi ya nchi yetu.....hiyo nayo ni topiki nyingine. Cha muhimu ni kufuatilia uendeshaji mbovu.....

      Delete
  71. Wengi wamechangia kuhusu upanuzi wa barabara lkn hilo kwa sasa linahitaji fedha Kubwa mno. Nidhamu ya madereva wengi ni mbovu Sana ukizingatia wamiliki wakubabaisha. Mimi maoni yangu ni mabasi yote ya mikoani yanatakiwa yawekewe GPS tracking systems ambayo itaonyesha overspeed ya kila basi na kuripotia kituo cha Polisi kilicho karibu. Faini lazima iwe Kubwa name onyo Kali kwa mmiliki wa basi mara tatu over speeding linafungiwa. This system is very cheap name wamiliki wote watafunga kwa gharama zao kupitia kampuni Kama U track, ISL name kadhalika. Central server itakuwa makao makuu ya polisi au Sumatra. Hoi ndio mwarobaini pekee wa kupunguza ajali nyingi za over speed. It is the best solution ever than speed governer. Then wamiliki watalipia Ada zq hio system.

    ReplyDelete
  72. Kama kweli tunataka haya yakome basi tusiogope gharama. Wazo langu ni kuwatunaishi katika karne ya 21 iliyojaa teknologia tena ni ya kisasa. Kwa wenzetu nchi zilizoendelea kuna utaratibu wa gari kuongozwa na satalite ili kumuwezesha dereva afike aendako bila ya kupotea.Mtandao wa satalite huwa unamuongoza na kum-mark yupo wapi na anatumia speed gani na pia anaongozwa kwa sauti ya mtu kama ananuona hasa yupo wapi..Pendekezo langu ni kuwa nasi Tanzania tuingie huko kupunguza ajali.Hiki chombo hakisemi uongo,kwa hivyo kila gari iwe ni sheria kutumia satalite ili kupimwa mwendo wake na ni satalite itakayoweka rekord ya kila nyendo ya gari popote ilipo barabarani tangu inaanza safari yake. Sasa wazembe kama hao katika picha mahakamani wakifikishwa hakuna ubushi maana recod yake ipo na ima faini kubwa kwa kosa la kwanza au la pili na kama atakuwa sugu basi hata kunyanganywa leseni yake.

    ReplyDelete
  73. 1.Wazo la kampuni kubwa ni zuri.Litasaidia sana kudhibiti ubora wa magari yanayotumika na mienendo ya madereva pia.
    2. Kuhusu rushwa ni lazima jamii ibadilike. Madereva na makondakta wengi huwa wanatoa chochote kumpa polisi mbele ya abiria na sijawahi kusikia abiria kwenda kuripoti kuwa tulipofika mahali fulani dereva wa gari tuliyopanda alitoa rushwa kwa polisi fulani ili gari yetu ipite. Mara nyingi ninaposafiri tukikutana na polisi anaefuata kanuni za kazi yake huwa nasikia baadhi ya abiria wakilalamika na kumshauri kondakta au dereva atoe chochote ili gari iruhusiwe wawahi safari zao. Hili la rushwa hili si jambo la mapolisi wala viongozi ni jambo la jamii.Tuanzie katika familia zetu, twende katika koo zetu na vitongoji vyetu, tupande tufike katika mitaa na vijiji hadi ngazi ya taifa. Rushwa bwana hii wala tusimlaumu mtu- tujilaumu sisi sote.Na kama unabisha hebu fikiria itakuwaje siku baba yako akihumkumiwa kupigwa risasi hadharani kwa kosa la kula rushwa. Utakuwa na furaha kwamba tumepiga hatua fulani katika kupambana na rushwa au majonzi kwamba umempoteza baba? Ukipata jibu la hapo ndio utajua ugumu wa tatizo la rushwa. Jamii yetu ni corrupt kwahiyo usitegemee viongozi au polisi kutokuwa na sifa hiyo ambayo tuliipalilia bila kujua. Mzizi wake upo katika kila familia. Kila mzazi na mkuu wa kaya akifanya kitu cha kupambana na rushwa basi baada ya miaka kadhaa rushwa itakuwa haipo- lakini sioni uwezekano wa kukomesha rushwa GHAFLA kwakuwa haikuanza ghafla. Mara nyingi vitu vinavyochukua siku nyingi ili kumea na kustawi huchukua pia siku nyingi kudhoofu na kufa.Tunapofikiria kukomesha rushwa tuwe na mikakati ya muda mfupi na muda mrefu kwakuwa ni kitu kimechukua muda hadi kustawi.

    ReplyDelete
  74. Mdau hapo juu nashukuru kwa mchango.Jamii kama jamii haiwezi kuamka from no where ikakemea Rushwa.Ndio maana tunakuwa na viongozi wa ku mobilize jamii. siku tukipata kiongozi wa kitaifa anaeweza kusimama kwa dhati kabisa kuziambia familia za kitanzania kwa nia moja sasa zichukie Rushwa hapo tutafanikiwa.hizo zinatakiwa kuwa sera na viongozi wenye nguvu kuzisimamia na kuitaarifu jamii ikatae Rushwa.Mimi na wewe tunachukia Rushwa lakini hatuna sauti ya kutosha kumobilize jamii badara ya kuishia kuandika kwenye blog amabazo mama yangu na baba yangu hazimfikii.
    Tanzania inahitaji Raisi mwenye nguvu kama ya baba wa Taifa (RIP) ili kuokoa janga la Rushwa ambalo limekuwa sehemu ya maisha ya viongozi wetu wa kitaifa.

    Mdau UK

    ReplyDelete
  75. AJALI BARABARANI (MAONI)

    Kwanza waombea DUA, ajali zilowakumba,
    MOLA akawachukuwa, macho yao kawafumba,
    PEPONI ende watuwa, ya milele yao nyumba,
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    Hakika tena si siri, bayana twashuhudia,
    Wafa kama utitiri, si mmoja kwa mamia,
    Ajali zimeshamiri, chanzo nini ngetwambia,
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    Wa madereva uzembe, bayana nnawambia,
    Mwenda mbio usiombe, nini mwakifukuzia?
    Mithili beba maembe, katu dhani abiria?
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    Sheria barabarani, zipo mwazipuuzia,
    Mwenda kama hamuoni, mbio kiongeza gia,
    Mwasahau humo ndani, kuna roho za mamia
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    Naja wana usalama, vipi macho lifumbia?
    Mwatanda njia nzima, maovu kishuhudia,
    Wajibika mmegoma, au rushwa mwavizia?
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    Madereva chonde chonde, kazi zenu zingatia,
    Angazeni zote pande, hakikisha ni sawia
    Kiwa shwari ndipo mwende, spidi walopangia,
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    Nazidi omba salama, wetu RABI tujalia,
    Twende turudi salama, mote nomojirandia,
    Pasitokee zahama, maafa katu sikia,
    Bado zazidi kuuwa, ajali barabarani.

    H.K

    ReplyDelete
  76. Michuzi shukrani sana kwa wazo hili la kuchangia kumbe kuna kero zinazowakabili wananchi ambazo watawala wetu hawana habari nazo.

    RUSHWA RUSHWA RUSHWA RUSHWA RUSHWA

    Mi nadhani mbili ama tatu hazina mashiko mbele ya jamii badara yake tuwe na Raisi mwenza atakaeshughulikia RUSHWA tu.

    ReplyDelete
  77. Ndio nimesoma points nyingi zilizoandikwa hapa na wachangiaji walio wengi,lakini kwa bahati mbaya sjakutana na yeyote yule aliyezungumzia suala la ulevi na uvutaji wa dawa za kulevya,hili nafikiri ni tatizo kubwa ambalo linachangia sana kwa hizi ajali za barabarani hapa nchini,madereva wengi hapa nchini siku hizi wameingilia ulevi na hata wengine kufikia kutumia madawa ya kulevya wakati wanapokuwa kazini.nafikiri wizara ianzishe drug and alcohol policy ili iweze kuwabaini wote wavunjaji wa sheria na kuwashughulikia pamoja na kunyang'anywa leseni zao za udereva pamoja na faini kubwa au kifungo.Peace

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna wachache wameya kugusia, kuna waliotaja viroba, bangi n.k. Haupo pekee yako.

      Delete
  78. Yote tisa kumi...madereva wengi hawajui kusoma wala kuandika...leseni za kupewa kwenye bar sangapi watajua solid line maana yake nini...kingine abiria wengi wanachangia ajali pia wanapenda mabasi yaende kasi...nakumbuka nilikuwa safarini dar to mwz basi lilikuwa likienda kasi sana nilimfuata dereva nikamwambia apunguze speed alikupunguza kutoka kwenye 100 mpaka 20 abiria wote wakaja juu dereva akasema kuna dada kasema naenda kasi. Wakaanza kunilaumu mimi alifanya makusudi ya kwenda very low speed .cha muhimu hao madereva wanatakiwa kwenda darasa la kupewa leseni na lesen ziwe na point kama nchi zingine. La sivyo watu wataendelea kufa kama kuku.

    ReplyDelete
  79. Nitazungumzia zaidi kuhusu Mabasi ya Abiria :
    1.Mabasi Chakavu au Used yasiruhusiwe kufanya biashara ya kubeba abiria hususan kwa umbali mrefu (country buses);
    2.Mabodi ya Mabasi ya Abiria yachunguzwe iwapo yamekidhi viwango vya usalama kwa abiria basi likiwa katika mwendo kasi na katika barabara zetu zenye ubora hafifu ; Iwe marufuku kwa chassis za malori kutumika kwa ajili ya kubeba abiria ;
    3. Uadilifu wa Askari wa Usalama Barabarani na Mamlaka husika katika kusimamia na kudhibiti Ubora wa Viwango vya Mabasi ya Abiria ni suala nyeti na muhimu sana .Idara ya Trafiki ni moja ya Taasisi za Umma zinazo lalamikiwa sana kwa Upokeaji wa Rushwa nchini . Dawa ya Tatizo hili inaeleweka.Atakaye zembea kuchukua hatua kwa wakati aachishwe kazi au kutolewa katika Kitengo chake .
    4.Umbali wa safari ukijulikana , na mwendo wa wastani wa basi la abiria ukijulikana(km. 80kph),ni kazi rahisi kujua Basi likiondoka Kituo kimoja katika muda gani , litawasili katika Kituo kinachofuatia muda wa majira gani au saa ngapi . Basi litakalo wasili mapema zaidi kuliko Muda wake kwa mujibu wa Ratiba ya Basi lake , ni wazi atakabiliwa na KOSA LA KU OVERSPEED , NA ADHABU KALI inapaswa kutolewa papo hapo bila kuzembea au kuendekeza Rushwa . Katika kila kituo lazima wawepo Askari wa Barabarani watakao simamia utaratibu huo .
    5. Umri utakao ruhusiwa kwa Dereva kubeba abiria au kuendesha mabasi ya abiria usiwe chini ya miaka 25.
    6.Madereva wote lazima wapimwe Macho kila baada ya miezi sita .
    7. Madereva wote lazima wapewe mafunzo ya UDEREVA WA KUJIHAMI (Defensive Driving).Dereva anapokuwa barabarani atambue haendeshi gari lake peke yake , bali anaendesha hata gari atakalo pishana nalo .Lazima achukue tahadhari zote za kutokiamini chombo chohocte cha moto atakacho pishana nacho .Lazima awe tayari wakati wote pindi Tayari lolote la gari litakapo pasuka au tukio la ghafla barabarani , akiwa na Uwezo kamili (Focus & Concetration)wa kulidhibiti Basi lake ,hata likipinduka basi lisilete madhara makubwa kwa abiria .
    8.Kampuni ya Mabasi ya Abiria itakayo kumbwa na ajali za mara kwa mara,inyang'anywe Leseni ya Kubeba Abiria .Dereva atakaye kuwa rekodi ndefu ya ajali za barabarani , anyang'anywe Leseni ya Udereva .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu point zako nzito. Asante kwa elimu

      Delete
  80. Kaka Michuzi, mwambie Rais, wewe upo karibu nae, kama kweli yupo serious na hii kitu basi na awekwe traffic mmoja katika kila gari kwa muda wa mienzi , ili wale madereva wajue maana na kuendesha kwa usalama, gari inapotoka na kurudi lazima awekwe mwana usalama barabari, na alipwe na hiyo kampuni , bila hivo hakuna kitakachofanyika wekeni tochi sijui vipunguza mwendo sijui ini vyote ni ulaji na kuwanufaisha watu na mwisho wa siku ajali pale pale,

    lazima serikali ijue kuwa madereva na askari wake barabari hawana nidhanimu! zaidi kuwa madereva wa mabasi na daladala wamewaweka kiganjani matrafiki wote wanaopita eneo hilo,

    Natamani kama ingewezekana Rais angeomba trafic wa nchi za wenzentu kama Uingereza hivi waje hapa kwa muda tuone kama ajali zitatokea si mijini wala huko vijijini

    Tumechoka kusikia na kuona watu wasio na hatia wanauliwa na hawa washenzi madereva!

    Wasalaam

    ReplyDelete
  81. Suluhisho la kudumu Kupunguza Ajali za Barabarani NI KUWA NA UTARATIBU PIA WA KUDUMU WA KUWAPIMA SAIKOLOJIA NA AFYA NYA AKILI MADEREVA KILA BAADA YA MIEZI MITATU!

    Afya ya binaadamu haina dhamana, inawezekana Dereva akaipata Leseni kipindi wakati akiwa mzima wa afya kwa akili lakini akawa chizi baadae, hivyo kwa uendeshaji wao mbaya wa kuleta ajali Madereva haina shaka labda tunaeneshwa na amchizi.

    Maana Ankali ni wazi ya kuwa AFYA YA AKILI NI SAWA NA HOMA YA EBOLA AMA DENGUE ambapo joto la mgonjwa hupanda na kushuka, hivyo ni MUHIMU SANA KUWAPIMA AFYA YA AKILI NA SAIKOLOJIA MARA KWA MARA MADEREVA HASA WA VYOMBO VYA ABIRIA !!!

    ReplyDelete
  82. Hongera mtunga shairi kwa ubunifu huu, ujumbe umefika

    ReplyDelete
  83. Ajali Barabarani
    Mwamgongo nakupongeza, Tungo yako uloanza
    Lazima kuwaeleza, wanazidi kutukwaza
    Roho zetu wanauza, madereva ni wakwanza
    Ajali barabarani,ufumbuzi nilazima

    Nikifikiri safari, roho yangu inasita
    Hawaweki tahadhari, madereva nawasuta
    Njiani wanazo shari, mwenzake akimpita
    Ajali barabarani, ufumbuzi nilazima

    Leseni kuzikagua, kabla hawajaondoka
    Vipimo kuvitambua, vya mwlini kadhalika
    Wanaweza kutumia,vilevi wakapinduka
    Ajali barabarani, ufumbuzi ni lazima

    Sote tuwe mabalozi, tofauti tukiona
    Siyo dereva mjuzi, kasi anapinda kona
    Lolote humuulizi, cha moto utakiona
    Ajali barabarani,ufumbuzi nilazima


    Polisi na waheshimu, usalama barabarani
    Roho zetu ni muhimu, rushwa haina thamani
    Rushwa ni sawa na sumu,baba yake ni shetani
    Ajali barabarani, Ufumbuzi ni lazima

    Mchuzi nakuusia, anzisha page ajali
    Video tukitupia, madereva wasojali
    Tutapiga kila njia, za karibu na za mbali
    Ajali barabarani, ufumbuzi nilazima

    Matajiri wahusishwe, ajali ikitokea
    gari lithibitishwe, kama limejiozea
    jamii itambulishwe, ripoti ikitokea
    ajali barabarani, fumbuzi nilazima

    Naikumbuka zamani, kipando cheye thamani
    Punda ninamtamani, awepo barabarani
    Atachelewa njiani, bora niwe na amani
    Ajali barabarani, Ufumbuzi nilazima

    Michuzi nakupongeza, mada hii kuiweka
    Tena ninapendekeza,wala isijefutika
    Hadi tukitokomeza,ajali zikatoweka
    Ajali barabarani, ufumbuzi ni lazima.

    Mama Muhammad
    shabanisekiete1@gmail.com

    ReplyDelete
  84. 1.Nakubali kuwa msimamo wa Rais wa nchi ni muhimu katika jitihada za kupambana na rushwa ambayo itasaidia kuboresha sekta ya usafirishaji na fani ya udereva na hatimaye kuchangia katika kupunguza ajali za barabarani. Hata hivyo ikumbukwe kuwa Rais ni kama mkuu wa kaya katika ngazi ya taifa, hivyo kazi yake itakuwa nyepesi kama atasaidiwa na wakuu wa kaya katika ngazi za chini ikiwemo ngazi ya familia.
    2. Ratiba ya kuondoka na kufika kwa basi katika vituo ni muhimu na ratiba hizo si kwamba hazipo, ZIPO. Ugumu upo katika ufuatiliaji hasa katika mfumo huu wa ushindani wa kibiashara ambapo kwa bahati mbaya sana wasafiri wengi huwa wanachukua kigezo cha kufika mapama kama ishara pekee ya ubora wa kampuni ya usafisi. Siku wasafiri watakapokubali kuwa kusafiri sio kufika mapema tu ila ni pamoja na kufika salama - tutakuwa tumepiga hatua kubwa sana katika sekta ya usafiri wa umma maana wakiona dereva anakimbia watamwajibisha mara moja na kama ataendesha taratibu kwa makusudi kama ilivyotokea kwa mdau hapo juu pia watamwajibisha. Hii haiwezi kutokea hadi wasafiri watapoelewa maana ya kusafiri na kuweka vigeza sahihi vya basi zuri la kufanya nalo safari na dereva mzuri wa kuendesha gari la abiria. Hii inaweza kuchangia kupunguza ajali maana kampuni isiyokidhi vigezo kwa mujibu wa mtazamo wa wasafiri itakosa abiria na hatimaye itakufa. Kwa uzoefu nilio nao, kampuni nyingi za mabasi ya abiria ambazo zimelegalega kwa sasa ni zile ambazo mabasi yake hayakimbii. Kwa namna hiyo ni vigumu sana kumshawishi dereva asikimbie wakati anajua kuwa asipofanya hivyo kampuni yake inajiweka katika hatari ya kukosa abiria. Kwahiyo ndugu zanguni pamoja na ulevi wa madereva, na kiburi cha madereva, na rushwa ya mapolisi wa barabarani,na ubovu wa magari, nk nk hebu tujiulize- nini maana ya safari kwetu sisi wasafiri wa mabasi? Tukipata jibu, tutaweka vigezo sahihi vya mabasi ya abiria na madereva wa mabasi hayo watakaotuwezesha tusafiri salama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...