DSC_0018
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akisoma risala ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu, wakuu wa shule mbalimbali, maafisa elimu na maofisa wa serikali kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za shirika hilo jijini Dar.

Na Mwandishi wetu
MRADI wa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu na sayansi na utamaduni (UNESCO) na kuendeshwa na wizara ya elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 umemalizika kwa mafanikio huku wito ukitolewa kutafutwa njia ya kuendeleza mradi huo.

Tangu awali mradi huo haukuelezwa kinaga ubaga unakuaje endelevu kama utaonekana kuwa na manufaa kwa taifa.

Akitoa maelezo ya kufungwa kwa mradi huo ambao uliojulikana kama Micro Science Kits (MSKs) kwa wadau wa elimu,wataalamu na maofisa wa serikali, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Bi. Zulmira Rodrigues aliwataka wadau hao kuzingatia mafanikio yaliyokuwapo,kuangalia changamoto zake na kuona namna ya kuendeleza mazuri ya mradi.

Mradi huo wa majaribio ulifanyika katika shule za mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Morogoro, Kigoma na Tanga kwa upande wa Tanzania Bara.

Aidha ilielezwa katika kikao hicho kilichofanyika ofisi za Unesco kwa lengo la kuufunga rasmi pamoja na malengo yake ya kuboresha elimu Tanzania kwa kuhakikisha masomo ya sayansi yanafundishwa kwa namna inavyotakiwa, tathmini ilionesha udhaifu wa kutokuwepo na mpango madhubuti wa kuendelezwa kwake.
DSC_0015
Mradi huu wa majaribio wa MSK ulilenga kukuza uwezo wa kufundisha masomo ya sayansi (baiolojia,kemia na fizikia) kwa shule ambazo hazina maabara kwakuzipatia visanduku vya majaribio pia uliendesha warsha mbalimbali ili kukuza uwezo wa matumizi ya zana zilizo katika mradi wa MSK pamoja na vitabu vya kufundishia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...