DSC_0009
Meneja wa Kituo cha Habari na Mawasiliano cha Redio Sengerema mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiutambulisha ujumbe wa wageni kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini kwa Wenyeviti wa bodi na mameneja wa redio za jamii nchini waliohudhuria warsha ya siku tano ya kuwajengea uwezo katika kuboresha masoko kwenye vituo vyao iliyofadhiliwa na shirika la maendeleo la Sweden (SIDA) na kuratibiwa na UNESCO.

Na Mwandishi Wetu, Sengerema
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kupitia Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) itaanza kutoa elimu inayohusu sheria ya vyama vya siasa na sheria ya gharama za uchaguzi kupitia redio za jamii ili kuwawezesha wananchi kutambua wajibu wao katika kulinda amani ya taifa kuelekea katika uchaguzi na wakati wa uchaguzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Beatrice Stephano wakati akizungumza na mameneja wa redio hizo katika warsha yao ya siku 5 iliyomalizika mwishoni mwa wiki mjini Sengerema.

Beatrice alikuwa akizungumzia mradi anaousimamia ambao umedhaminiwa na UNDP kupitia UNESCO kwa ajili ya kuelimisha umma wa watanzania kupitia redio za jamii katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi 2015.

Alisema uamuzi wa kutumia redio za jamii unatokana na redio hizo kuwafikia wananchi wengi zaidi, hali ambayo wadau katika masuala ya demokrasia wameona kwamba inaweza kutumika kuboresha zaidi uelewa wananchi.
DSC_0081
Mratibu wa Mradi wa kuimarisha Demokrasia na Amani (DEP) kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini, Bi. Beatrice Stephano (wa pili kushoto) akizungumza na mameneja wa redio za jamii nchini wanaohudhuria warsha ya siku tano inayofanyika kwenye kituo cha Habari na Mawasiliano cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza kuhusiana na ofisi yake kufanya kazi kwa pamoja na redio za jamii nchini katika kutoa elimu kwa umma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...