Madaraka Nyerere, Mtoto wa Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere, pamoja na Mwanamuziki Mzalendo Vitali Maembe wameteuliwa na shirika lisilo la kiserikali Culture and Development East Africa (CDEA) kuwa mabalozi wa kushiriki kampeni ya kupanda Mlima Kilimanjaro ili kuhamasisha jamii kuchangia ujenzi wa jukwaa la sanaa na ubunifu jijini Dar es Salaam.

Kampeni hiyo ya kupanda Mlima Kilimanjaro imeandaliwa na CDEA kupitia njia ya kupanda Mlima Kilimanjaro kuanzia Septemba 7 hadi 13 mwaka huu ili kujenga jukwaa na sanaa na ubunifu litakalowapa fursa wasanii na vijana kukutana, kufikiri na kubuni kwa pamoja ambapo mawazo ya kisayansi yatakutana na sanaa na pia sanaa kukutana na taaluma nyinginezo nyingi.

Mkurugenzi Mtendaji wa CDEA, Ayeta Wangusa anasema “ili kufanikisha kampeni yetu ya mwaka mmoja tuliyoipa jina la ‘FUN FOR FUNDS’, tumeona ni vyema kupanda mlima Kilimanjaro kwa kumtumia Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya CDEA, Madaraka Nyerere pamoja na Vitalis Maembe ambaye ni mwanamuziki mzalendo”.
DSC_0045
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na Balozi wa kampeni ya "Fun For Funds", Madaraka Nyerere (wa tatu kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam dhumuni lake la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za jukwaa la sanaa na ubunifu ili kukuza vipaji vya vijana kupitia mafunzo mbalimbali ya sanaa na kutoa muongozo wa jinsi ya kuanzisha wazo la ubunifu na kulikamilisha.Na kuongeza pia vijana wataunganishwa na majukwaa mengine kama hili kwa nchi za Afrika Mashariki kama vile The Nest, PAWA 254 na Creative Garage yote ya Kenya na Africa Sanaa Kollective ya Uganda.
DSC_0067
Balozi wa kampeni ya kuchangisha fedha, “FUN FOR FUNDS” mwanamuziki mzalendo mzee wa ‘Sumu ya Teja’ , Vitali Maembe akizungumza na waandishi wa habari ambapo amewataka wasanii wenzake kuungana kuwa kitu kimoja katika kukuza utamaduni wetu kwa kubadilishana uzoefu wa kazi zao bila choyo.
DSC_0104
Mjumbe wa bodi ya shirika lisilo la kiserikali la Culture and Development East Africa (CDEA), Rose Haji Mwalimu akitoa rai kwa waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo (hawapo pichani) na kuwataka kutumia kalamu zao vizuri na kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...