Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
      
Watu wawili wameuawa Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika matukio mawili tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema tukio la kwanza limetokea mnamo tarehe 20/09/2014 majira ya saa 23:30hrs katika Kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma ambapo mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MWAJUMA D/O CHOMOLA mwenye umri wa miaka 48, Mgogo mkazi wa Mzogole aliuawa kwa kupigwa na Rungu tumboni upande wa kushoto na mumewake aliyefahamika kwa jina la RICHARD S/O KODI mwenye umri wa miaka 55, Mhehe mkulima na mkazi wa kijiji cha Mzogole Wilayani Mpwapwa Mkoani  Dodoma ambaye nae aliuawa tarehe 21/09/2014 majira ya saa 09:00hrs baada ya kushambuliwa na wananchi waliojichukulia sheria mkononi na alifariki dunia akiwa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa baada ya wananchi hao kupata taarifa kuwa mwanamke huyo kafariki kutokana na kipigo cha mume wake.

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha mauaji hayo ni wivu wa mapenzi kwani RICHARD aliuawa na wananchi baada ya kumuua MWAJUMA ambaye alikuwa mkewake aliyekuwa akiishi nae, baada ya kuchelewa kurudi kutoka kwenye sherehe iliyokuwa hapo kijijini akidhani kuwa ameenda kwenye masuala mengine.

Aidha Kamanda MISIME amesema wananchi waliojichukulia sheria mkononi bado wanatafutwa ili wafikishwe mahakamani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kitendo cha mume kuua mke wake ni cha kulaaniwa na ni kosa la jinai. Ingawa ni vizuri wangemuachia jamaa huyu sheria ichukue mkondo wake, hii iwe ni funzo kwa wanaume wanaoua wake zao kwamba jamii haikubaliano nao. Hata wale wanaokandamiza na kunyanyasa wake zao waache tabia hiyo mbaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...