Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Mwenge-
Tegeta utakaofanyika tarehe 1 Oktoba 2014.
Ufunguzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta wenye urefu wa Kilomita 12.9, utafanyika
kuanzia saa nne asubuhi katika eneo la Lugalo njia panda ya Kawe.
Upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa
Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es
Salaam.
Taarifa hii imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini(GCU)
Wizara ya Ujenzi
Duh!! Barabara nzuri lakini hamna taa!! Ni hatari sana nyakati za usiku. Mh. Magufuri hapo vipi???
ReplyDeletekwanini anazindua nusnusu? mbona haina taa wala miti katikati? tuwe serious kuutengeneza mji wetu
ReplyDeleteBarabara ni nzuri lakini wameinyima Taa,na ni hatari sana kwa vile mpka sasa barabara ikiwa ata bado haijafunguliwa tumeshuhudia ajali nyingi na za kutisha tena nyingine zikitokea mchana
ReplyDeleteMsongamano wa magari katika barabara hii angalau umepungua kwa kupanuliwa barabara hii.
ReplyDeleteMwanzo mzuri lakini ilikuondoa tatizo la foleni kwa muda mrefu ujao ilibidi kuwa na lane nyingine ya zaidi,yaani;kuwe na three lane one way.Hilo eneo la katikati nikubwa mno lingetosha kupata lane mmoja ya ziada.
ReplyDeleteTaa jamani muhimu barabara hiyo ni kero usiku.
ReplyDeleteHii barabara imejengwa na wajapani sasa taa zimekosekana vipi.
ReplyDelete