Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza
ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York.
Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York,
Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani,
Washington, D.C.
Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya
10 ikiwa ni pamoja na kuhutubia Baraza Kuu wakati wa Majadiliano ya Jumla (
General Debate) yaliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi 27 na Septemba 29
hadi Oktoba Mosi, mwaka huu, 2014.
Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia Baraza
hilo mchana wa Alhamisi ijayo, Septemba 25, 2014. Mkutano wa 69 wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa utaanza Septemba 16 hadi Desemba 24, mwaka huu,
Miongoni mwa mikutano mingine muhimu ambayo Rais Kikwete atashiriki
ni pamoja na kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa
Umoja wa Afrika (AU) Kuhusu Mazingira (CAHOSC) na Mkutano wa Wakuu wa
Nchi Kuhusu Mazingira ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),
Mheshimiwa Ban Ki Moon.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
16 Septemba , 2014.
Mh Rais Safari hii jaribu kuhutubia baraza kuu kwa lugha ya kiswahili. Muhimu kukipa kipaumbele kiswahili yeye ndio head of state ataifanya lugha yetu kutambulika zaidi ndio kuitangaza.Viongozi wote wa nchi Mfano French Pres. always ana hutubia kwa french lakini anazungumza English vizuri sana. Tafadhari Mh Rais tangaza lugha yetu mwaka huu toa hutubia baraza kuu kwa lugha yetu ya kiswahili. Asante
ReplyDeleteKigulu London
Maoni yako yamechanganya lugha, hivyo huonekani kukienzi kiswahili kama unavyotaka ueleweke kwa wasomaji. Maneno ya kiingereza uliyotumia ''head of state'' na ''always'' hayakupaswa kutumika hapo kwa mtu anayesisitiza kiswahili kienziwe
ReplyDeleteNaungana na hapo juu. Atakipaisha Kiswahili kwa kweli. Kila la heri safarini. Selina
ReplyDelete