Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Eliya
Ntandu akifungua mafunzo ya siku sita ya maofisa watakaoshiriki katika Tathmini
ya kina ya Matukio Muhimu ya Mwanadamu. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa
Shughuli za Kitakwimu wa NBS, Bi Aldegunda Komba, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk.
Albina Chuwa, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi Emmy Hudson na Kamishna wa
Sensa, Hajjat Amina Mrisho Said.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Bi. Emmy
Hudson akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa RITA katika tathmini.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu, Dk. Albina Chuwa akitoa maelezo kuhusu ushiriki wa NBS katika
tathmini.
Picha ya Mgeni Rasmi na washirki wa
Mafunzo.
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
(RITA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wanaendesha mafunzo
ya siku sita kwa maofisa watakaoshirki kufanya tathmini ya kina ya Usajili na Takwimu
za matukio muhimu ya mwanadamu ambayo ni Vizazi, Vifo, Ndoa na talaka. Mafunzo
hayo yamefunguliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Eliya Ntandu Jana
Jumanne tarehe 2 Septemba 2014 na yanafanyika katika ukumbi wa 88 Motel, Mkoani
Morogoro.
Mafunzo hayo yanawashirikisha maofisa
kutoka taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya usajili wa wananchi ikiwa
ni maandalizi kwa ajili ya kuwapa uwezo wa kufanya tathmini ya kina ya mifumo
na sheria zilizopo zinazohusika na usajili wa matukio muhimu ya mwanadamu
ambayo ni Vizazi, vifo, Ndoa na Talaka .
Tathmini inategemewa kufanyika tarehe
15 -30 Septemba 2014 katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini na maofisa
waliopewa mafunzo wataweza kukusanya taarifa katika vituo vya tiba, vituo vya
polisi, ofisi za wasajili wa wilaya, ofisi za kata, nyumba za ibada na katika
makazi ya wananchi.
Matokeo
ya Tathmini yanategemewa kutoa mwelekeo katika mchakato wa kuweka vipaumbele na
mipango ya utekelezaji wa mfumo thabiti wa usajili wa raia na utoaji wa takwimu
za matukio muhimu, mfumo utakaokuwa kiungo muhimu katika utekelezaji wa utawala
bora na pia chanzo cha msingi cha takwimu za matukio kama vizazi, ndoa, talaka
na vifo na sababu zake.
RITA NA NBS wanafanya tathimini hii ikiwa
ni utekelezaji wa moja ya maazimio ya
Mkutano Mawaziri wanaohusika na masuala ya usajili wa raia wa nchi
wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Mwaka 2012 katika Jiji la Duban,
Afrika ya Kusini. Kwa mujibu wa azimio hilo kila nchi mwanachama inatakiwa
kufanya tathmini hii na kuwasilisha matokeo yake katika kikao kama hicho
kinachotegemewa kufanyika mwanzoni mwa
mwaka ujao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...