Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Utawala Bora wa
 klabu ya Young Africans Wakili Sam Mapande - kulia

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema utapinga maamuzi ya kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji kuhusiana na maamuzi yake ya kumtangaza mchezaji wake, Emmanuel Okwi kuwa huru.
Sam Mapande amesema kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo ambayo yanakinzana na shitaka zima la mchezaji huyo. Mapande amesema kuwa kamati ya TFF imeamua sakata la Okwi kinyume na malalamiko yao kwani hakukuwa na lalamiko la mchezaji huyo wa Uganda kuhusiana na malipo ya fedha zake za usajili.Alisema kuwa cha kushangaza, kamati hiyo ya TFF iliamua kusikiliza kesi ambayo haikuwa mbele yao na kutoa maamuzi ambayo hata wao wameshangazwa nayo.
“Kwanza kesi yenyewe ilikuwa haijamalizika, walituambia tuwasilishe vielelezo kuhusiana na kitendo cha mchezaji huyo kufanya mazungumzo na klabu ya Misri, lakini cha kushangaza maamuzi yametolewa, hili limetushangaza sana,” alisema Mapande.
Alisema kuwa mazingira yalikuwa yameandaliwa kuibeba Simba na Okwi kwani hata malalamiko yao kwa Simba hayakusikilizwa. “Malalamiko yetu yalikuwa wazi kabisa, yapo kimaandishi, hatukuwai kulalamikiwa, suala la fedha za usajili la Okwi limetoka wapi, kama lilikuwepo, mbona hatujajulishwa kimaandishi kama utaratibu ulivyo,” alisema.
Alisema kuwa Kamati hiyo kumruhusu mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Zacharia Hans Pope ambaye pia ni mwenyekiti wakamati ya usajili ya Simba kuwemo katika kikao hicho kinyume na taratibu za Fifa kupitia kifungu namba 19 kinachoeleza mgongano wa kimaslah

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...