SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Serengeti Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Shinyanga mjini ndani ya Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Uhuru iliyopo mjini humo.
Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Shinyanga wengi wao wameonesha hali ya kuelewa baadhi ya mafunzo na mbinu hizo na kuaahidi kuzifanyia kazi ipasavyo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuyatimiza malengo yao waliojiwekea.
 Meneja wa Maxcom Africa, ‘Max malipo’,  Bernard Munubi  ambaye aliwapatia mbinu za mafanikio na namna ya kujikwamua kiuchumi kupitia mashine za Max Malipo ambazo kwa kiasi kikubwa sasa zimeweza kuwapatia ajira wakazi wengi nchini.
Naye mzungumzaji kutoka  kampuni ya GSI Tanzania,Afisa Mwanadamizi wa kampuni hiyo Tanzania,Pius Mikongoti akizungumza kwenye semina hiyo ya fursa ikiwemo na kuwapa mbinu za kujikwamua kupitia kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...