Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje akiwakaribisha
wajumbe wa mkutano wa kujadili ushirikishwaji wazawa (local content)
katika sekta ya madini uliofanyika jijini Mwanza hivi karibuni. Waliokaa
meza kuu kutoka kushoto ni Kamishna Msaidizi Kitengo cha Uchumi na
Biashara, Salim Salim, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijila na
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele.
Mwanasheria wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Rose Mponguliana
akiwasilisha mada kuhusu uwajibikaji wa Shirika hilo katika suala la
ushirikishwaji wazawa wakati wa mkutano baina ya Serikali na Makampuni
ya Madini uliofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.
Wajumbe wa Mkutano baina ya Serikali na Makampuni ya Madini uliojadili
ushirikishwaji wazawa katika sekta ya madini wakisikiliza hotuba ya
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Ndalo Kulwijila (hayupo
pichani).
Wajumbe wa Mkutano baina ya Serikali na Makampuni ya Madini uliojadili
ushirikishwaji wazawa katika sekta ya madini wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo katika Hoteli ya Gold
Crest jijini Mwanza hivi karibuni. Kutoka Kushoto waliokaa ni Kaimu
Kamishna Msaidizi wa Madini Sehemu ya Uongezaji Thamani Madini Latifa
Mtoro, Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje, Katibu Tawala
Mkoa wa Mwanza Ndalo Kulwijila na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John
Henjewele.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...