Serikali kwa kupitia mkataba wa Motrial wa mwaka 1987 imejipanga thabiti katika kuhakikisha
kuwa tatizo la uharibifu wa tabaka la ozini linapata suluhu Tanzania.
Mkurugenzi wa Manzingira Ofisi ya Makam wa Rais, Dk. Julius Ningu aliyasema hayo ofisini
kwake katika mahojiano na waandishi wa habari alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya hatua ya
serikali katika kudhibiti uharibifu wa tabaka la Ozoni.
Dk. Ningu alisema kuwa kabla ya mwaka 1985 wanasayansi waligundua kumomonyoka kwa
tabaka la Ozoni, umomonyokaji huo ulipelekea wanasayansi kutoa mapendekezo kwenye
umoja wa mataifa, na umoja wa mataifa wakaamua kuitisha mkutano wa nchi wanachama
mwaka 1985 na mkutano ulifanyika Vienna-Australia ambako ndiko uliko anza mkataba wa
Vienna wenye lengo la kusitisha uzalishaji wa gesi zinazo momonyooa tabaka la Ozoni.
Sanjari nahayo alisema kuwa Serikali imejipanga vyema katika kuakikisha kuwa inatoa elimu
kwa Umma juu ya swala la gesi ambazo sirafiki kwa mazingira na aliaainisha kuwa mpaka sasa
wataalamu wapatao 400 walipatiwa mafunzo ya jinsi ya kugundua gesi zisizo rafiki pamoja na
kuweza kutambua na kufichua watu wanao tumia gesi hatarishi.
Akibainisha baadhi ya vifaa vyenye mchanganyiko wa gesi hatarishi Dk. Ningu alisema kuwa
air fresh, rangi za kupaka kwenye nyumba na magari, viyoyozi mitumba, majokofu mitumba na
madawa ya kuulia wadudu mashambani na manyumbani nyingi zinachakachuliwa na kuwa na
kemikali hizo hatarishi.
Katika kubainisha madhara ya uharibifu wa tabaka la Ozoni DK. Ningu alisema kuwa yapo
madhara mengi na makubwa yatokanayo na uharibifu wa tabaka la Ozoni kwa viumbe hai na
mimea, alibainisha madhara hayo ni kama vile saratani ya ngozi, utindio wa ubongo, na mtoto
wajicho.
Kwa upande wake Mkurungezi msaidizi wa Idara ya Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais, Bi
Magdalena Mtengu alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na taasi mbali mbali imefanikiwa
kutoa elimu juu ya swala zima la matumizi ya gesi rafiki kwa tabaka la Ozoni, aidha alisema
kuwa mpaka sasa tayari mpango huo umesha ingia kwenye baadhi ya vyuo vya ufundi kama
vile Veta Changombe Dar es salaam, Veta Moshi, Chuo cha Uvuvi Nyegezi Mwanza, Chuo
cha ufundi Arusha, Dar es salaam Institute of Technology, Taasisi ya Sayansi na Technology
Karume Zanzibar, Chuo Kikuu cha Sayansi na Technology Mbeya, Veta JKT, Veta YMCA,
Kihonda Morogoro ,Taasisi ya Taafa ya Usafirishaji, na Taasisi ya Uvuvi Bagamoyo.
Katika kupambana na uharibifu wa tabaka la Ozoni serikali imekumbana na changa moto mbali
mbali kama vile ufahamu mdogo wa wafanya biashara wetu juu ya gesi rafiki na zisizo rafiki
kwa tabaka la Ozoni, suala la uelewa mdogo wa wanachi juu ya gesi hatarishi kwa matumizi.
Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dk. Julius Ningu akizungumzia uharibifu wa Tabaka la Ozoni utokanao na matumizi ya gesi zisizo rafiki kwa Mazingira, Ofisini kwake leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Saalam.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Magladena Mtengu, akitoa ufanunuzi kuhusu mikakati inayo chukuliwa na Serikali katika kuelimisha umma juu ya uharibifu wa Tabaka la Ozoni inayosababishwa na matumizi ya gesi hatarishi kwa Mazingira akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Saalam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...