Viongozi wa vilabu vya timu zinazotarajia kushiriki kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) yanayotarajiwa kuanza Septemba 27 mjini Morogoro wametakiwa kusajili timu zao mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza hapo baadae wa kushindwa kusajiliwa kutokana na mapungufu ya timu zao.

Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo aliyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya mashindano ya SHIMIWI uliofanyika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo.

Bw.Katembo alizitaka timu zinazotumia wachezaji walioajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu kuacha tabia hiyo na badala yake watumie wachezaji wenye mikataba ya mwaka mmoja na kuendelea ili kuepuka tatizo la kutumia mamluki kwenye timu zao.

"Tafuteni wachezaji ambao ni wafanyakazi katika Ofisi nyingine za Serikali kama timu zenu zina mapungufu ya wachezaji" alisema Bw. Katembo.

Naye Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka aliwataka viongozi hao kutoa taarifa ya timu ambazo hazitashiriki mashindano hayo mapema iwezekanavyo ili kuepuka gharama zinazotumika katika maandalizi ya timu zao.

"Timu ambazo hazitaweza kushiriki ziwe wazi kusema hazishiriki kwa sababu SHIMIWI inatumia gharama nyingi kwenye maandalizi" alisema Bw.Makuka.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe wa SHIMIWI na viongozi wa vilabu vya timu mbalimbali kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mashirika ya Umma na Halmashauri za Wilaya.
Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo akifungua mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya Mashindano ya SHIMIWI uliofanyika katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto kwake ni Katibu wa SHIMIWI Bw. Moshi Makuka (wa pili) na wajumbe wa SHIMIWI wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Katibu wa SHIMIWI Bw.Moshi Makuka (wa pili kutoka kushoto) akitoa mada wakati wa mkutano maalumu wa kupanga ratiba ya timu zitakazoshiriki kwenye SHIMIWI mwaka huu katika ukumbi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam mapema leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa SHIMIWI Taifa Bw. Ally Katembo na wengine ni wajumbe wa SHIMIWI Taifa wakifuatilia mada.
Mmoja wa Wajumbe wa SHIMIWI akishiriki katika zoezi la kupanga makundi mbalimbali katika ratiba ya michezo ya SHIMIWI.
Kamati maalumu ikipanga ratiba ya makundi mbalimbali katika michezo ya mpira wa miguu,mpira wa pete, bao,karata, riadha,kuvuta kamba na kurusha tufe katika michezo ya SHIMIWI.
Baadhi ya wajumbe wa SHIMIWI na Viongozi wa Vilabu vya Michezo wakifuatilia mada.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...