Shiriko lisilo la Kiserikali la Farm Africa kwa kushirikiana na wakulima wa uyoga wa wilaya za Mbulu na Babati wiki iliyopita waliandaa siku maalum ya kula uyoga kwa wakazi wa wilaya hizo.

Tukio hilo lilifanyika katika katika kitongoji cha Magugu wilayani Babati ambapo wakazi walipata nafasi ya kuonja aina mbalimbali za mapishi ya uyoga.Wakulima 15 wa uyoga walio katika mradi wa Misitu wa Farm Africa walishiriki shughuli hiyo kwa kupika na kugawa  bure uyoga uliopikwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Kilimo cha uyoga ni njia mbadala iliyopo kwenye mradi wa misitu ambapo wakulima badala ya kukata miti kwa ajili ya kuitumia kwa kuwapatia kipato, wanapanda uyoga ambao wanauuza na kuwaingizia kipato.
Siku ya kuonja uyoga ilikuwa na madhumuni ya kuwahamasisha wakazi wa Babati kuhusu faida za kilimo cha uyoga, mapishi yake na jinsi kilimo hicho kinavyoweza kuwaingizia kipato cha ziada.
 Ni wakati wa kula uyoga!
 Wadau wakipatiwa mafunzo ya kilimo cha uyoga na wakulima walio kwenye mradi wa misitu wa Farm Africa
 Wakulima wakionyesha jinsi uyoga unavyooteshwa
 Wananchi wakiburudika na rosti ya uyoga
Wananchi wakipakuliwa rosti ya uyoga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...